KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Monday 25 May 2015

UNESCO YASISITIZA UPENDO KWA WATOTO WENYE ALBINISM

DSC_0945
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues (katikati) akiambatana na Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir (kushoto) walipotembelea shule msingi Mitindo ya watoto wenye ulemavu wa ngozi, macho na masikio iliyopo katika wilaya ya Misungwi nje kidogo ya jiji la Mwanza. Kulia ni Mtaalamu wa Jinsia na Haki za Binadamu kutoka UNESCO Tanzania, Bi. Annica Moore.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

………………………………………………………..
Na Modewjiblog team
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)Tanzania, Zulmira Rodrigues amesisitiza umuhimu wa kuwapenda watoto wenye ulemavu wa ngozi katika jamii baadala ya kuwatenga .Zulmira alisema hayo alipotembelea watoto wenye ulemavu wa ngozi katika shule ya msingi ya Mitindo iliyopo katika wilaya ya Misungwi nje kidogo ya jiji la Mwanza mwishoni mwa jumaShule hiyo ya serikali ina wanafunzi zaidi ya 1000 wakimo wenye ulemavu 202 .Kati yao 81 ni wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi ambao wanahifadhiwa na serikali katika shule hiyo maasa 24 kufuatia wimbi la mauaji la watu wenye ulemavu wa ngozi katika mikoa ya kanda ya ziwa .Hata hivyo Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa UNESCO Tanzania alionekana kupatwa huzuni kubwa kutokana hali ya maisha ya watoto hao .“ Nimehuzunika sana (I am so sad). Sio tabia ya watu wa Afrika kuwatenga watu wanyonge (weak people)”alisema huku akitokwa na machozi mara baada ya kuwatembelea watoto hao na kuongea nao pamoja na uongozi wa shule hiyo.Alisema ni muhimu watoto hao wenye ulemavu wa ngozi kuwa wanavaa nguo za mikono mirefu ili kuwakinga na jua kwa ajili ya kulinda afya zao.Hata hivyo Zulmira alipongeza jitihada zinazofanywa na serikali ya Tanzania kulinda watu wenye ulemavu wa ngozi na kutoa wito kwa wadau wote kuunga mkono juhudi hizo.

No comments:

Post a Comment