KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Thursday 6 August 2015

WAGOMBEA 21 WA NAFASI YA UBUNGE MBAGALA WAMPINGA MWENZAO ALIYESHINDA

Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula
WAGOMBEA ubunge 21 wa Jimbo la Mbagala wamesema kuna hatari Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikalipoteza jimbo hilo kutokana ukiukwaji wa taratibu za kura ya maoni, zilizofanywa na mgombea mwenzao aliyeongoza katika kura za maoni.
Jimbo hilo la Mbagala  lenye Kata 10 ni jimbo jipya la uchaguzi ambalo linakadiriwa na kuwa na watu zaidi ya 600,00 kulingana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.
Akizungumza  na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, mmoja wa wagombea hao, Ali Makwilo, alisema kuwa endapo mgombea aliyeongoza jina lake litarudihwa na vikao vya ngazi ya juu, basi wataamua kumsusa kwa kutomfanyia kampeni.
“Hatuelewi kwa nini wametangaza matokeo wakati tawi la Mianzini halijapiga kura pia hawajatupa nakala ya matokeo kutokana na hali hiyo tunagomea matokeo ya kura hizo,”alisema Makwilo.
Alisema hofu hiyo inatokana na uvunjifu wa haki na vitendo vilivyokithiri matumizi makubwa ya rushwa, kwamba wanpinga ushindi aliyoupata Issa Mangungu kwani ni batili.
“Mshindi aligawa rushwa ya Madera kwa akina mama na tisheti kwa vijana, aligawa kadi batili za CCM kwa wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF), ugawaji rushwa ya pesa,”alisema Makwilo.
Naye mgombea mwingine Mohamed Mchekwi, alisema sheria ya chama hicho iko wazi, zinasema kuwa kila wakati wa kampeni  hizo wagombea wote wanatakiwa kupanda gari moja.
Alisema cha kushangaza mwenzao alikuwa akitumia magari matano huku yakiwa yamejaza wapambe wake na amekuwa akitangulia katika vituo akifanya kampeni peke yake.
Mchekwi, alisema kuwa matatizo yote hayo yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na Makatibu wa Matawi kutokana na vitendo vyao vya kukubali kupokea rushwa kwa ajili ya kumpendelea mgombea aliyeshinda.
 “Tunakiomba chama kupitia vikao vyake halali vya kuchuja majina visimrudishe mshindi kutokana na hofu ya kupoteza jimbo la Mbagala kwa wapinzani kutokana ushindi aliyoupata mgombea huyu,”alisema Makwilo.
Aliongeza kuwa chama hicho hakina matatizo na hakina cho cha kufundisha vitendo vinavyokwenda kinyume cha maadili, lakini kimekuwa kikichafuliwa na wahuni wachache wenye uchu wa madaraka.
Aidha, alisema wanatambua taratibu za chama zinavyoshughulikia matatizo kama haya, lakini katika hili tayari walikwisha lifikisha katika ngazi ya wilaya kichama tangu awali hata hivyo hakuna hatua zilizochukuliwa.

Agosti Mosi chama hicho kilifanya mchakato wa kura za maoni kwa ajili ya kumpata mgombea atakayepeperusha bendera ya CCM katika Uchaguzi Mkuu mnamo Oktoba 25, ambao utavishirikisha vyama vingi.

No comments:

Post a Comment