BAADHI ya vijana mkoani Dar es Salaam, wamemtaka Naibu Waziri wa
Sayansi na Teknolojia, January Makamba kutokata tamaa baada ya kukosa nafasi ya
kuteuliwa kuwa mgombea wa nafasi ya urais ndani ya Chama Chama Mapinduzi (CCM).
Vijana hao walisema hivyo, baada ya kukamilia mkutano wa kumpata
mgombe wa nafasi hiyo ndani ya chama hicho, mjini Dododoma jana, ambapo Dk. John Magufuli
ameteuliwa kupeperusha bendera ya CCM itakapopambana na wapinzani katika
uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Wakizungumza na Tanzania Daima jijini, kwa nyakati tofauti jana,
vijana hao, walisema kwa hatua aliyofika ya wagombea watatano kati ya 38, katika
uteuzi huo inaonesha dhahiri kuwa Watanzania wanahitaji uongozi wa kizazi
kipya.
Walisema, hivyo kwa vile wanaamini kuwa uwezo wa kuongoza nchi hii
anao, kilichochangia akose nafasi hiyo ni kutokana na umri wake mdogo, ambao baadhi
ya wajumbe waliopewa dhamana ya kuteua kuangalia zaidi umri wa mgombea,
akibainisha mwenye umri mkubwa huwa ndio wananmpa nafasi zaidi.
Stephen James mkazi wa Gongolamboto, alisema kuwa Makamba, hana haja
ya kusikitika na kukata tamaa kwa vile umri wake bado unaruhusu kugombea nafasi
hiyo panapo maajiliwa ifikapo mwaka 2025 kwani atakuwa na miaka 51, cha msingi
ajipange kuanzia sasa.
“Nafarijika kumuona Makamba akiwa hazina kubwa ndani ya CCM hivyo
umefika wakati kwa wakongwe wa chama hicho kuwaamini vijana kwa vile
wakiaminiwa na kuthaminiwa uwezo wao, kutoka ngazi ya chini hadi taifa wanaweza
kufanya mambo makubwa nchini,”alisema James.
Halima, Kisambu, alisema lazima wazee wa chama hicho wabadili msimamo
katika kuachia nafasi za uongozi kwa kizazi kipya bila ya mizengwe hali
itakayowafanya vijana wote wa CCM na wengine kuamini kuwa chama hicho ni chao
wote.
Hivi karibuni Naibu Waziri huyo, alikaririwa navyombo vya habari,
akisema hana kinyongo na anawaheshimu
baadhi ya wagombea na yuko tayari kufanyakazi na mgombea yeyote kwa
ajili ya kuendelea kukijenga na kukiimarisha Chama chao na kutatua changamoto
za Watanzania.
No comments:
Post a Comment