Mgombea ubunge Jimbo la Kawe, Mdee |
Mgombea wa ubunge Jimbo la Ubungo, Kubenea |
Halikadhalika wameitaka kumaliza
kasoro mbalimbali zilizojitokeza katika maeneo mengine nchini.
Wakazi jijini
walijiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura kwa kutumia mfumo wa kieletroniki
Biometric Voters Registration (BVR), kuanzia Julay 22 hadi Ogasti 4 mwaka huu.
Wakizungumza na waandishi
wa habari jijini jana, wagombea hao walisema kuwa baada ya kujiandikisha, zoezi
hilo la uhakiki, lilitakiwa kuanza Ogasti 18 mwaka huu lakini hadi sasa
halijaanza na hawajui kinachoendelea.
Mdee, alisema wakiwa wadau
wauchaguzi wamebaini kuwa hadi sasa wapiga kura wao hawajahakikiwa katika maeneo,
hali inayowatia shaka, kwa vile hata
madaftaari yenyewe hayajafika katika Halmashauri na Kata kwa ajili ya ukaguzi.
“Sasa tunaitaka NEC ieleze
kwa kina na kidagaubaga kuwa ni lini haswa zoezi la uhakiki wa daftari hilo
utaanza,”alisema Mdee.
Mdee, pia aliitaka NEC
kutoa maelekezo kwa wasimamizi wa uchaguzi kuwa madaftari ya majina yote ya
wapiga kura ya pelekwe kwenye vituo waliko jiandikisha baadala ya kuwataka waende
katika ofisi ya Kata.
“Itakuwa ni vigumu kwa
wananchi wa vituo vyote katika Kata husika kwenda kukagua majina yao kwenye
ofisi za kata, jambo ambalo halitawezekana kwa vile siku zenyewe zilizopangwa
ni chache, kutakuwa na mkusanyiko mkubwa, hivyo ni vyema majina hayo
yakapelekwa na kubadikwa kwenye vituo vyao.
“Ni rai yetu mashine za BVR
zikawekwa karibu na mitaa kwamba endapo kutabainika kasoro katika vituo husika basi
ziweze kushuhulikiwa haraka ,”alisema Mdee.
Aliongeza, kwa kuiambia NEC
kuwa wao wakiwa wagombea wa mkoa huo hawatakubali kuona wapiga kura wao wanakukosa
haki yao ya kupiga kura kutokana na uzembe wa tume.
Akizungumzia kasoro
zilizojitokeza katika maeneo mengine nchini ambako tume imekwisha hakiki majina
nchini Mdee, alisema kuwa kuna baadhi ya wapiga kura majina yao hayakuonekana.
Alisema kuna maeneo ambako
watu wamejiandikisha zaidi ya 3000 lakini cha kushangaza baadhi ya majina
hayako katika daftari lakini wananchi hao wanavyo vitambulisho (vichinjio),
vyao.
“Unajua uchaguzi wa safari
hii unaupinzani mkali sasa kukosekana kwa wapiga kura kiasi chochote ni jambo
la hatari sana,”alisema Mdee.
Alisema, kuna mchezo mchafu
unaofanywa na wakurugenzi hivyo wanaitaka tume hiyo kuhakikisha kuwa inamaliza
kasoro hizo haraka, ambazo zinaweza kuja kuwanyima haki ya kupiga kura wananchi
nakuzua vurugu.
Naye Kubenea, alisema kuwa
ziko taarifa zinazodai kuwa kuna mpango wa wizi wa kura kwa kuongeza idadi ya
kura za urais na udiwani, ambapo mpango huo unaratibiwa na baadhi ya watendaji
wa NEC, ambao siyo waadilifu.
“Tunashangaa kuwa hadi sasa
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum kuwa hadi sasa hawajamsikia akitoa kalipio kali kuhusu
shahada hizo kali kwa kutumia itelejensia kwa watu hao wa CCM wanaodaiwa kuwa
na shahada hizo,”alisema Kubenea.
Alisema kuwa hadi wakati
huu wakielekea katika uchaguzi huo wana mashaka na tume kwasababu baadhi ya
viongozi wa tume hiyo uwadilifu wao unatiliwa shaka katika kusimamia kazi hiyo.
Kubenea, alisema kutokana
na wasiwasi huo wanamtaka Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damiani Lubuva, ili aondoke
vizuri katika ofisi hiyo ni lazima asimamie sheria na ahakikishe kuwa uchaguzi
huo unakuwa huru na haki.
“Kama alivyosema mwenzangu hawatakubali
kwa wapiga kura wao waliokesha, na miswaki, ndoo za maji, vyungu, pawa, nyungo
ili kusubiri kujiandikisha leo wasipige kura huku wakiwa
wamejiandikisha,”alisema Kubenea.
Alisema vinginevyo mafuriko
au maporomoko ya wananchi waliyokuikataa CCM kama watanyimwa haki yakupiga kura
na NEC basi itambue kuwa itaingiza nchi katika machafuko.
MWISHO
No comments:
Post a Comment