JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limesema ndegevita moja imeanguka katika
uwanja wa ndege wa kijeshi uliyoko Mwanza wakati zikifanya mazoezi ya kivita.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es salaam leo,
Meja wa Jeshi hilo, Joseph Masanja, alisema ndegevita hizo zilikuwa katika
mazoezi ya kwaida ya kivita.
Alisema ajali hiyo ilitokea wakati rubani wa ndege hiyo
Meja Piter Lyamungu alipokuwa akijiandaa kuruka, ilitokea ndege nyingine (ndegemnyama),
ikaingia katika moja ya injini zake na
kusababisha ndegevita kuwaka moto.
Meja Masanja, alisema hata hivyo rubani wa ndegenita hiyo
alipoona ndege yake inawaka moto alifanikiwa kujirusha nje ya ndege hiyo kwa
kutumia vifaa maalumu.
Alisema baada ya kutumia vifaa hivyo alifanikiwa kuokoa
maisha yake ingawa amepata majeraha katika mguu wake wakati kujiokoa.
Meja Masanja, alisema hali ya rubani huyo inaendelea vizuri
na anaendelea na matibabu ya kawaida.
Alitoa rai kwa wananchi kuwa wasiwe na hofu kwani ajali
iliyotokea ilikuwa ni ajali ya kawaida na kwamba waendelee na shughuli za kama
kawaida.
Meja Masanja aliongeza kwa kusema kuwa sehemu ilipoamgukia
ndegevita hiyo haikuleta madhara yeyote ya binadamu, nyumba wala miundombinu.
No comments:
Post a Comment