WABUNGE wa Mkoa wa
Geita wametupiwa lawama kutokana na kushindwa kujitokeza katika tukio la mauaji
ya mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (Albino), Yohana Bahati.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea
hivi karibuni ambapo baadaye mwili wa mtoto huyo aliyetekwa ukujakuepatikana
ukiwa umekatwa miguu na mikono yote na kiwiliwili chake kufukiwa shambani
katika kitongoji cha mapinduzi kijiji cha Rumasa ndani ya hifadhi ya msitu wa
Biharamulo wilaya ya Chato mkoani Geita.
Wakizungumza na mwandishi wa habari
hizi katika maeneo ya Posta jijini Dar es Salaam, wakazi wa jiji hili, walisema
ni jambo la aibu kwa bunge hao kukaa kimya kama vile hawanatarifa na
kilichotokea.
Salome Julius, alisema kuwa
kushindwa kwa wabunge hao kujitokeza kunadhihirisha ukweli kwamba mauaji ya
Albino yanaratibiwa na wanasiasa wenye tama ya vyeo, wakishirikiana na waganga
wasio jail uhai wa mwanadamu mwingine kutokana na tama ya fedha.
“Hadi leo hakuna hata mbunge mmoja
ambaye amekwisha jitokeza na kuonesha kuwa kilichotokea hakiwahusu na
wamenyamaza kimya,”alisema Salome.
Khadija Jumanne, alisema pamoja na
mtoto kunyofolewa viungo vyake bado mama wa mtoto hyo, Ester Jonas alijeruhiwa
kwa mapanga wakati akipigania maisha ya Yohana.
Alisema, hivi sasa Ester amelazwa
lakini cha kushangaza hadi leo ikiwa zimepita zaidi ya wiki mbili hakuna hata
Mbunge mmoja ambaye amekwenda kumjulia hali kitendo ambacho kinazidisha
wasiwasi kwa wananchi kuamini kuwa kweli
wanasiasa ndio wanaoratibu unyama huo.
“Niwaombe wabunge wa Geita wakae chini
chini na kisha wafikie uawamuzi wa busara wakwenda kumjulia hali Estera kitendo
ambacho kitwajengea imani kwa wanachi,”alisema Khadija.
Hivi karibuni Mtoto huyo wa mwaka
mmoja alitekwa nyumbani akiwa amebebwa na mama yake mzazi, Esther ambaye alijeruhiwa
katika tukio hilo kwa kupigwa panga usoni.
Kwa mujibu Kamanda wa polisi mkoa wa
Geita, Joseph Konyo, mwili huo ulipatikana katika shamba la mahindi lisilo
rasmi kutokana na kulimwa ndani ya hifadhi ya msitu wa Biharamulo wilayani
Chato.
Kamanda SACP Joseph Konyo alisema
maiti ya mtoto huyo iligunduliwa na mpita njia katika shamba la mahindi
lililopo kitongoji cha tatu kutoka nyumbani kwao, baada ya kuona kipande cha
nguo yenye damu ambapo alipiga yowe lililowakusanya wanakijiji ndipo walifukua
shimo alipokuwa kafukiwa na kukutwa akiwa hana mikono na miguu yote.
Wakati huo huo hali ya mama Ester
Jonas ambaye ni mama wa mtoto huyo bado ni tete na madaktari wa hospitali ya
rufaa Bugando wanaendelea na juhudi za kuhakikisha hali yake inaimarika.
No comments:
Post a Comment