Katibu Mkuu wa ACT, Mwigamba katikati ni Mwenyekiti wa chama hicho Mambo na mwanachama mwingine |
CHAMA cha Uwazi na Mabadiliko (ACT-Tanzania),
kimefanya marekebisho ya Katiba kwa kuingiza cheo kipya cha Kiongozi Mkuu wa
chama ambaye atakuwa mwenye kauli ya mwisho kuhusu masuala yote ya chama.
Katibu Mkuu wa chama hicho, Samson Mwigamba alitoa
kauli hiyo, wakati alipozungumza na wandishi wa habari kuhusu kikao cha Kamati
Kuu kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Alisema, wamefikia hiyo kwa vile nafasi hiyo haiko
katiba katiba wanayo itumia sasa, baada ya kukamilika watatoa taarifa kwa
wanachama wake wanaotaka kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi unaofanyika leo.
“Nafasi nyingine zote za kitaifa yani Mwenyekiti
Taifa, Makamu mwenyekiti wa Bara na Visiwani na wengine hizo ziko katikaKatiba
ya Chama ambapo wagombea wengi tayari wamekwishakua fomu kwa ajili ya kugombea
nafasi hizo,”alisema Mwigamba.
Mwigamba, alisema kiongozi huyo ndio atakuwa na
fursa ya kugombea urais wakati wa Uchaguzi Mkuu kila utakapofika.
“Kuanzishwa kwa nafasi hii kutasaidia kumuepusha
rais wan chi kuwa na kofia mbili bali awe kiongozi wa nchi tu,”
Mwigamba alifafanua kwa kusema kuwa baada ya agenda
ya marekebisho hayo, kitiba hiyo itaanisha tofauti ya za utendaji wa kiongozi mkuu
wa chama na mwenyekiti.
Aidha, mkutano huo ulitarajiwa pia kutoa taarifa
za utendaji wa chama hicho tangu kilipoanza, kadhalika walifungua Kikao cha
Halmashari Kuu.
Mwenyekiti wa chama hicho, Shaba Mambo, alisema
wakati umefika sasa kwa chama hicho, kufanya uchaguzi ili kupata vuongozi wa
kudumu kwani tangu kilipoanzishwa, hata baada ya kupata usajili wa kudumu
kilikuwa kikiongozwa na viongozi wa muda.
Leo chama hicho, kitafanya uchaguzi wa viongozi
wake wa ngazi zote ambapo kesho kitazinduliwa huyo ikiwa ni ishiria kuwa kimeanza safari.
Uzinduzi huo utahudhuriwa na viongozi mbalimbali
wa kisiasa wa ndani na nje, pia na taasisi nyingingine.
No comments:
Post a Comment