Dk. Bilal, akizungumza na wandishi wa habari, wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Mifuko ya Kijamii ambalo ni la siku mbili, likianzia leo na kumalizika kesho. NA MWANDISHI WETU |
MAKAMU wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, amesema serikali
itahakikisha kila mstaafu analipwa mafao yake kutoka katika Mifuko yao ya Hifadhi ya Jamii.
Bilal, alisema hayo jijini Dar es Salaam jana, wakati
akizindua kongamano la siku mbili la wadau wa mifuko hiyo inayosimamiwa na
Mamlaka ya Udhibiti wa Usalama wa Mifuko (SSRA).
Bilal alisema serikali inatambua kazi nzuri iliyofanywa na
wastaafu ambao wengi wao walifanya kazi kwa uaminifu mkubwa na hatimaye
kuchangia maendeleo nchini.
“Mifuko hii
tumeianzisha makusudi ili kuwalea wastaafu baada ya kuwa wamefanya kazi nzuri
katika nchi yetu hivyo hawastahili kuachwa wahangaike,” alisema Dk. Bilal.
Aliwataka wasimamizi wa mifuko hiyo kutumia mkutano huo
kama chachu itakayozidi kuwajengea uwezo wa kuelewa maeneo mbalimbali ya
uwekezaji.
“Hivi sasa mifuko hii inawekeza kwa ajili ya kujitunisha na
lengo kubwa ikilenga kuwasaidia wanachama wake katika masuala mbalimbali ya
kijamii ikiwemo ajira,” alisema.
Naye Mkaguzi Mkuu wa Mifuko hiyo, Peter Mberwa alisema,
hivi sasa wametoa muongozo utatumika kisheria na mifuko hiyo ikilinganishwa na
awali ambapo walikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa sheria.
No comments:
Post a Comment