JESHI la Polisi mkoani Pwani linawashikilia watu sita raia
wa Malawi kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Kamishina Mwandamizi
(SACP) Ulrich Matei alisema watu hao walikamatwa juzi eneo la mizani ya Maili moja
Kibaha kutoka Zambia kwenda Dar es salam.
Kamanda Matei alisema kuwa katika tukio hilo raia hao wa
Malawi walikua wakisafiria gari lenye namba za usajili BQ7828 aina ya
Mitsubishi Fuso iliyokua ikitokea Zambia kwenda Dar es salam usiku wa kuamkia
Machi 03.
Waliokamatwa katika tukio hilo ni Saam Manda(19), Meshack
Nigata(22), Juniour Mngonje(26), Isack Ndamba (20), Weziel Longwe (21) na
Mource Zawinja(35).
Kamanda Matei alisema watuhumiwa hao watakabidhiwa idara ya
uhamiaji na hatua za kisheria dhidi yao zitachukuliwa.
Wakati huo huo, watu wawili wamepoteza maisha katika ajali
ya barabarani iliyotokea juzi majira ya saa 11 jioni huko Ndagoni kata ya
Baleni Wilaya ya Mafia.
Katika tukio hilo gari lenye namba za usajili T842 ASC aina
ya Mitsubish Fuso ikiendeshwa na Salehe Yahaya iliacha njia na kupinduka .
Kamanda Matei amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kuwataja waliopoteza maisha kuwa ni pamoja Deodatus Sapila (21) na Said Simba
(25).
Tukio jingine katika Wilaya ya Bagamoyo, Kombo Zuberi (18) ambaye
ni mvuvi amekutwa akiwa amefariki dunia chooni huku mwili wake ukiwa na alama
za kujidunga sindano kwenye kiwiko cha mkono wa kulia.
Taarifa ya tukio hilo inabainisha kuwa kando ya mwili wa
marehemu ilikutwa bomba la sindano lenye dawa za kulevya na pakti ndogo ya dawa
hizo.
No comments:
Post a Comment