KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Wednesday 4 March 2015

MAKAMBA: NAMFAHAMU RAIS AJAE

Katibu Mkuu wa zamani CCM,Yusuf Makamba akilia baada ya kutoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa Kapteni Komba.

Na Mwandishi Wetu
KATIBU Mkuu wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rajabu Yusufu Makamba amesema hadi sasa anamfahamu Rais wa nchi hii hajae.

Makamba alisema hayo juzi wakati alipokuwa kwenye shughuli ya kuuaga mwili wa maerehemu Kepteni John Komba, ambaye alifariki Februari 28 mwaka huu baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari.

Makamba alikuwa akijibu swali la mwandishi wa habari aliyekuwa akitaka kujua kama msimamo wake kisisasa na marehemu Kepteni Komba ilikuwa ikifanana kuhusu urais katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Alisema haikuwa sahihi kuzungumzia suala hilo katika eneo lile la viwanja Karimjee, kwa vile walikuwa pale kwa ajili ya maombolezi ya msiba Kepteni Komba ambaye pia alikuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi.

“Sikuja kuzungumza masuala ya uchaguzi tuko hapa kwa ajili ya msiba hivyo niacheni katika hilo,”alisema Makamba.

Hata hivyo, Makamba alisema kama kuna mwandishi anataka kujuaRais ajaye basi ni vema akamtafuta wakati mwingine tena akimfuata nyumbani kwake.

Katibu huyo, Mkuu wa zamani, alijigamba kuwa hadi sasa anamfahamu Rais wan chi hii ajae, lakini bila ya kufafanua.

“Rais ajae mimi na mfahamu kama nilivyokwambia ukitaka kumjua njoo nyumbani kwangu Tegeta tutazungumza na nitakuambia,”alisema Makamba.

No comments:

Post a Comment