Mwenyekiti wa CCM, mkoani Shinyanga, Mgeja |
OFISI ya Waziri Mkuu imesema katika hatua za awali imetoa msaada wa
kuwakoa watu waliokumbwa na mafuriko yiliyosababishwa na mvua iliyoambatana na
upepo mkali, aliyotokea juzi katika Kata Mwakata wilayani Kahama mkoani
Shinyanga.
Akizungumza na Blog jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Msaidizi wa
Kitengo cha Maafa, Naima Mrisho, alisema hadi sasa kitengo hicho tayari
kimekwishachukua hatua za dharura.
Alisema linapotokea tukio kama hilo
hatua wanazochukuwa ni kuwaokoa majeruhi ambao wamebaki katika eneo la maafa.
Alisema kitengo hicho tayari kimeshatoa msaada wa vyakula na mahema
kwa ajili ya kuwahifadhi baadhi ya familia ambazo makazi yao yamebomolewa na mvua hiyo.
“Tunawasiliana na wadau wengine ili wasaidie watu hao walipatwa na
maafa hayo yaliyotokana na mvua kubwa. Pia ofisi inajipanga zaidi,” alisema
Naima.
Mgeja atoa pole
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga, Khamis
Mgeja, aliwapa pole wale wote waliokumbwa na maafa hayo, huku akiwataka wawe na
subira.
“Mimi natokea safarini kwenye msiba wa Kepteni John Komba lakini
kikubwa ni kuwapa pole wote walioathirika na janga hilo , kwa kweli ni lakusikitisha,” alisema
Mgeja.
Alisema wanaishukuru serikali kwani iliweza kufika haraka katika
tukio hilo ,
ambapo pia waliyaomba mashirika mbalimbali kufika hapo kwa lengo la kujitolea
msaada.
Alisema serikali iko pamoja na wananchi na kila jitihada zinafanyika
ili iweze kuwasidia wananchi hao.
No comments:
Post a Comment