KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Monday 6 April 2015

KITUO CHA POLISI KIMARA KUREKEBISHIWA MUDA WA KUFANYAKAZI


JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema litarekebisha kituo cha Polisi cha Kimara kilichopo Kata ya Saranga, wilayani Kinondoni ili kiweze kufanya kazi saa 24.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Kamanda wa Kanda 
Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema maboresho hayo yanatokana na wingi wa wakazi wa eneno hilo.

Alisema mbali na kituo hicho kufanyiwa marekebisho, vituo vingine navyo vitafanyiwa  marekebisho, ili viweze kuhudumia wananchi  muda wote.

“Tunajipanga kuboresha vituo vya polisi ambavyo kwa sasa vinafungwa kuanzia saa 12 jioni na kufunguliwa saa 12 asubuhi,” alisema Kamanda Kova.

Alisema Jeshi la Polisi halijachoka kuwasaka watu wanaosadikiwa  kuwa ni majambazi  ambao wanavamia vituo vya polisi  na kusababisha mauaji huku wakichukua silaha.

Aliongeza kuwa kazi ya Jeshi la Polisi ni kupambana na wahalifu wanaosumbua raia  na kuwafanya waishi kwa hofu.
Kamanda Kova alieleza jeshi hilo linaendelea na uchunguzi na kuwaomba wananchi watoe ushirikiano wa kutosha kuwafichua wahalifu, ili kuendeleza amani nchini.

 “Tukiwakamata tutawahoji  kwa nini wavamie vituo vya polisi na kuchukua silaha, wanazipeleka wapi wakati ni watu wa kawaida,” alieleza Kamanda Kova.

No comments:

Post a Comment