KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Monday 6 April 2015

CRDB, MANYARA YATOA MSAADA WA SH. MIL. 5

Mkurugenzi Mtendaji, Dk. Kimei

BENKI ya CRDB, Tawi la Babati mkoani Manyara imetoa msaada wa sh. milioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa maabara za shule 33 za sekondari za wilayani Hanang’ ikiwa ni katika jitihada za kuunga mkono kauli ya Rais Jakaya Kikwete ya kutaka kujengwa kwa maabara kwenye shule za sekondari za hapa nchini.

Akikabidhi fedha hizo juzi kwa Mbunge wa Hanang’, Dk. Mary Nagu, Meneja wa tawi hilo, Ronald Paul alisema, fedha hizo zitasaidia kununua mifuko 10 ya saruji kwa kila shule hizo za 

sekondari katika wilaya hiyo.
Paul alisema, wameamua kutoa mchango huo ili kurudisha fadhila kwa jamii inayowazunguka hasa katika kusaidia sekta ya elimu na afya nchini.

“Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei, nakabidhi msaada huu ambao nina imani katika kila sekondari za wilaya hii zitaweza kunufaika kupitia msaada huo,” alisema.


Akipokea msaada huo, Dk. Nagu kwa niaba ya wananchi wa wilaya hiyo aliishukuru benki hiyo kwa msaada huo ambao anatarajia utumike katika shughuli hiyo maalum hatua itakayosaidia 

No comments:

Post a Comment