VIJANA 22 wanaofanyabiashara ya kusafirisha abiria kwa kutumia pikipiki (bodaaboda), wameweza kumiliki pikipiki baada ya kuthubutu kuchukua mkopo wenye riba nafuu wa vyombo hivyo kutoka kampuni Benet Group & Microfinance Ltd.
Vijana hao walifikia hatua
hiyo baada ya kubaini kuwa pikipiki walizokuwa wakifanyaia kazi huku zikiwa sio
mali yao zilikuwa zikiwarudisha nyuma kimaendeleo kwani hesabu waliyotakiwa
kupeleka kwa mmiliki ilikuwa haiendani kipato wanachopata kwa siku.
Akizungumza na wandishi wa
habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Mtemi
Mahungucillo, alisema Benet Group& Microfinance Ltd imechukua dhamana
katika Kampuni ya Fekon ya China, ili iwawezeshe vijana kwa kuwapatia pikipiki
hizo kwa mkopo wenye riba nafuu ukilinganisha na kwingine.
Alisema lengola kutoa
mikopo hiyo kwa vijana ina lenga kuwawezesha vijana kujiari pia kumfanya kijana
huyo aweze kumiliki pikipiki yake.
“Jumla ya mkopo huo wa
pikipiki ni sh. milioni 2,356,000 ambao mkopaji atawajibika kuulipa ndani ya
miezi nane kwa kulipa ama kwa kila wiki sh. 58,000 au kwa mwezi sh
232,000,”alisema Mahungucillo.
Mahungucillo, alisema
kampuni hiyo inatoa fursa hiyo kwa mtu mbinafsi, kikundi, taasisi ya chama,
dini na vikundi vya walemavu, vyote hivyo viewe vimesajiliwa kisheria.
Hata hivyo, mkurugenzi huyo
alisema fursa hiyo inatolewa kwa wakazi wa jijini Dar es Salaam na Pwani.
Akizungumzia mkopo huo,
Mohamed Mzuki, alisema anashukuru kupata pikipiki hiyo, kwa vile yeye ni
mkulima huko Ifakara mkoani Morogoro anaamini itamsaidia katika shughuli zake
za kilimo kama vile kubebea pembejeo na mazao wakati wa kuyarudisha nyumbani.
Naye Juma Kilangilo, ambaye
ni dereva wa bodaboda maeneo ya Mabibo, alisema mwanzo alikuwa akiendesha ya
mtu ambayo ilikuwa aikimbana katika malipo ya siku, lakini naamini kwa kupata
yake anaamini itamkwamua katika matatizo yake ya uchumi na kumletea maendeleo
kwenye familia yake.
No comments:
Post a Comment