MKURUGENZI Mtendaji wa Sikika,
Irinei Kiria amewatahadharisha Watanzania kuwa wajiandae na kiama endapo Bunge
litaridhia kupitisha bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ya sh bilioni.
37 katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2015/16.
Kiria alisema hivyo, baada
ya kubaini katika kipndi cha miaka mine iliyopita, bajeti ya dawa muhimu na
vifaatiba imekuwa ikishuka na kusababisha ongezeko kubwa la uhaba wa dawa
muhimu huku waathirika wakuu wakiwa wananchi wa hali chini.
Mkurugenzi huyo, alitoa
kauli hiyo jijini Dare es Salaam jana, wakati alipozungumza na wandishi wa
habari kwa kuitaka serikali iongeze Bajeti ya Dawa Muhimu na Vifaatiba kwa
mwaka 2015/16.
“Kwa mwaka wa fedha 2015/16
bajeti imeshuka kwa kiasi kikubwa sana ikilinganishwa na mahitaji ambayo ni
zaidi ya bilioni 500 ilihali bajeti iliyotengwa ni bilioni 37 tu,”alisema Kiria
Kiria, alisema ili
kuepukana na tatizo hilo la uhaba wa dawa, taasisi hiyo inapendekeza serikali
iongeze fedha zakutosha kwa ajili ya dawa muhimu na vifaatiba katika mwaka huo.
Alisema ongezeko hilo,
litahakikisha upatikanaji wa dawanchini unaongezeka kufikia asilimia 80 katika
mwaka 2016 kama inavyotarajiwa na mpango wa matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Aidha, alisema kuwa
serikali kupitia wizara za fedha na afya zinapaswa kuhakikisha fedha
zilizotengwa kwa ajili ya dawa muhimu na vifaatiba zinatolewa kwa wakati ili
kupunguza uhaba wa dawa nchini.
Vilevile alisema Wizara ya
Afya itoe mwongozo na mikakati inayoeleweka na kuwezekana katika kutumia mapato
ya afya ya halmashauri kwa ajili ya ununuzi wa dawa muhimu na vifaatiba.
Kiria, alisema kuwa pia ni
vyema miongozo hiyo ikaweka wazi mifumo ya uwazi na uwajibikaji.
“Tunaelewa kwamba Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii inapanga kutumia mapato ya mbadala/fedha za uchangiaji
katika kusaidia bajeti ya dawa muhimu na vifaatiba katika mwaka wa fedha
205/16.
“Kwa kutumia fedha hizi ili
kuziba pengo ni kitu kisichowezekana kwa sasa kwa sababu makusanyo na matumizi
ya fedha hizi hazijulikani na hakuna taarifa kuwa ni kwa kiasi gani fedha hizi
zinaweza kuziba pengo la upungufu wa Bajeti,”alisema Kiria.
Akizungumzia kushuka kwa
bajeti hiyo katika kipindi cha miaka minne, Kiria, alisema mahitaji yamekuwa
yakiongezeka huku bajeti ikishuka, mathalani mahitaji ya dawa muhimu na
vifaatiba yameongezeka kutoka sh. bilioni 188 (2011/12), hadi sh. bilioni 577
(2014/15).
Kiria, alisema bajeti hiyo
inayopangwa imepungua kutoka sh. bilioni 123.6 (2011/12), hadi bilioni 70.5 kwa mwaka wa fedha wa 2014/15.
Alisema licha ya kupungua
kwa fedha zilizotengwa, serikali imeakuwa ikitoa fedha hizo pungufu ya zile
ilizoahidi.
Mfano mwaka 2011/12),
iliahidi sh. bilioni 123.6 lakini ikatoa bilioni 98 tu na mwaka wa fedha
(2014/2015), iliahidi 70.5 hadi sasa imetoa sh. bilioni 33.3.
No comments:
Post a Comment