KAULI ya Mwenyekiti wa Chama Mapinduzi (CCM), Rais ya Jakaya Kikwete, ya kukitaka chama chake kuteua wagombea wanaokubalika kwa watu na kwamba zama za kutegemea jina la chama kuwa zimepitwa na wakati, zimeungwa mkono na baadhi ya makada wa chama hicho.
Rais Kikwete alitoa kauli
hiyo juzi wakati akifungua Mkutano wa
Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM mjini Dodoma.
Wakizungumza na wandishi, kwa nyakati tofauti leo, makada wa chama hicho, Hamis Mgeja na Mgana
Msindai, walisema, kauli hiyo inaonesha ni jinsi gani ndani ya CCM kuna ukomavu
wa kisiasa.
Msindai, alisema hivyo kwa
kuwa kauli ya Rais inaondoa mawazo yaliyojengeka vichwani mwa baadhi ya makada
kwamba kiongozi mzuri ni yule anayekubalika kwa viongozi wa chama hicho.“Kauli ya Rais siyo mbaya
kwa sababu amesema achaguliwe mgombea anayekubalika na watu, hapo sina tatizo,
kiongozi anayekuabalika na watu kwa mfano katika makada wote waliojitokeza
kugombea, tayari watu wanaye mtu anayekubalika hivyo sio vyema wakachaguliwa mgombea
viongozi wa chama,”alisema Msindai.
Msindai, alisema kiongozi
anayefaa kwa wakati wa sasa ni yule amabye anao uwezo wa kutoa uwamuzi ambao
unalenga kukigeuza chama na kukirudisha kwanye mstari na kuijenga Tanzania
yenye maendeleo yanayogusa wananchi wote.
Khamis Mgeja, alisema kauli
hiyo imewapa faraja, kwamba mwenyekiti wao amekuwa ni mwuelewa na amewatangulia
kusoma alama za nyakati.
“Kauli ambazo zinaonesha
ndani ya CCM kuna ukomavu wa mtazamo na kwa kweli kiongozi atakaye kipa chama
ushindi ni yule anayekubalika na wananchi na wala sio matakwa ya viongozi,”alisema Mgeja.
Mgeja, alisema anaimani
kuwa kauili hiyo ni njema kwani wamekuwa wakilizungumza kwa muda mrefu kwamba
kiongozi wa kweli atatokana na matakwa ya wananchi hilo kwa muda mrefu sasa.
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu
wa Chama hicho, Yusuf Makamba, alisema inakuwa ni vigumu kwake kutoa maoni yake
kuhusu kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wake.
“Hayo ni maneno ya
mwenyekiti unataka niseme nini yangekuwa yamesemwa na mtu mwingine ungeniuliza
maoni yangu lakini mwenyekiti? Sina la kusema elewa masuala ya siasa nimestaafu,
sasa nimekuwa mfugaji njoo une ng’ombe wangu mmoja anaitwa Madale amjifungua
narudia hayo mambo nimestaafu.
Alisema mambo ya siasa hivi
sasa amewaachia wanasiasa kama vile Januari Makamba hao ndio wanaoweza
kuzungumzia siasa, akibainisha kwamba aulizwe maswali yanayohusu ufugaji.
Juzi mjini Dodoma, Rais
Kikwete alisema zama za kushinda kwa mazoea kwamba mgombea akishateuliwa na CCM
lazima ashinde, zimepitwa na wakati.
“Tusijidanganye kwamba
anayeteuliwa ni lazima ashinde, tutateua mgombea anayekubalika na wengi,
vinginevyo tutaula wa chuya,”alisema Kikwete.
Hata hivyo, Rais Kikwete
alisema katika kufanya uteuzi, lazima wazingatie masilahi ya chama kwanza, mtu
baadaye.
No comments:
Post a Comment