Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Madabida |
MWENYEKITI wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, amewataka wanachama
wenye nia ya kuwania nafasi kama vile ubunge na udiwani kufuata kanuni na
utaratibu wa chama.
Madabida, alitoa kauli hiyo
baada ya kutakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu madai kwamba diwani wa Kata ya Kijichi
Anderson Charles amekuwa akijihusisha katika kumpitisha pitisha mmoja wa makada
ambaye hivi sasa ni Mbunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Jimbo la
Kigamboni ambalo liko chini ya Faustine Ndugulile.
Akizungumza jijini leo, Madabida, kwanza alimtaka mwandishi amueleze alikozipata
taarifa hizo.
Alisema licha ya kuwataka wanachama
hao kufuta taratibu pia aliwashauri wote wenye taarifa amabazo hazina mashaka
kuhusu wanachama wanaovunja taratibu na kanuni za chama kwa kujipitishapitisha
kwenye majimbo yenye wabunge wa chama hicho, kuwafanya wakose raha na kushindwa
kutekeleza ahadi zao wazifikishe wakiwataja wanaofanya hivyo.
Madabida, alisema chama
hakitakuwa tayari kuzifanyiakazi taarifa za madai kama hayo, ambazo hazitaji
chanzo halisi kwa vile zinaonekana kuwa ni za majungu.
Naye diwani wa Kijichi,
Charles, alisema taarifa hizo ni za uzushi kwani kama zingekuwa za kweli basi kutokana
na utaratibu wa chama chake anaamini kuwa angefikishwa kwenye Kamati ya Maadililakini
kwa kuwa ni za uongo ndio maana hajafikishwa kwenye kamati hiyo.
“Wewe umeambiwa na mbunge
mwenyewe, kama hajakuambia ni uongo na hizo ni za kwako wewe, na amini,”alisema
Charles.
Aidha, alishangazwa na
kauli kwmba anamsaidia mbunge huyo wa Afrika Mashariki kwa makubaliano kuwa
akifanikiwa kuupata ubunge wajimbo hilo basi atamsaidia kupata umeya, jambo
alisema ili uwe meya ni lazima kwanza upate udiwani.
“Tuhuma hizi ni za kitoto
kwa mtu anayejua ni kwamba mbunge hana uwezo wa kumpa diwani umea isitoshe mimi
nilikuwa meneja wa kampeni wa mbunge wa Kigamboni,”alisema.
Awali, taarifa hizo zilitolewa na baadhi ya wanachama watiifu kwamba mbunge huyo
ambaye kwa sasa yuko nje ya nchi kwamba diwani huyo amekuwa mstari wa mbele
kuona mbunge wao anakosa nafasi hiyo katika kura za maoni za chama hicho.
Hivi karibuni Mbunge wa
Ilala Mussa Zungu, alikariliwa na vyombo vya habari akisema kwamba hatishwi na baadhi
wanachama wenzake wanaoutaka ubunge katika jimbo hilo kupitia kwenye mitandao ya
kijamii kama vile Fecebook.
No comments:
Post a Comment