KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Friday 29 May 2015

DK. BILAL, KUZINDUA KALENDA YA KIISLAM, JUNI 7 MWAKA HUU

MAKAMU wa Rais,  Dk. Mohammed Gharib Bilal, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kalenda ya kiislamu.
Uzinduzi huo utafanyika Juni 7, mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa Karimjee, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya APICO Tanzania Limited, Sheikh Habibu Masano, alisema lengo la kuandaa kalenda hiyo ni kutokana na idadi kubwa ya kiislam kutojua tarehe za kiislamu.
Alisema waislamu wengi hawafahamu tarehe wala miezi ya kiislamu, hivyo kalenda hiyo itamuongoza kujua.
Alisema katika uzinduzi huo wamealikwa watu mbalimbali wakiwemo wachungaji, maaskofu na wanachuoni kutoka nchi mbalimbali ambazo ni Zambia, Malawi na Uganda.
“Waislamu wengi hawajui tarehe wala miezi ya kiislamu, mara nyingi wakitaka kufahamu wanauliza kwa masheikh, kwahiyo ili kuwarahisishia kalenda hii itawaongoza….haijahusisha waislamu tu bali jamii yote, na itatumiwa na dini zote,” alisema.
Aliongeza kuwa katika kuitengeneza kalenda hiyo, wametumia miaka 2, na haina miezi mifupi, kila mwezi unaishia tarehe 30.

No comments:

Post a Comment