KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Friday 10 July 2015

DK. GEOFREY MALISA, ATANGAZA KUGOMBEA URAS 2015

KADA wa Chama Cha Kijamii (CCK), Dk. Geofrey Malisa, ametangaza nia na kuomba kuteuliwa na chama chake kwa ajili ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Dk. Malisa ambaye ni Mhadhili katika Chuo cha Mtakatifu Stephen Mwika mkoani Kilimanjaro alisema hatua hatua yake hiyo imekuja baada ya chama hicho kuaza kugawa fomu kwa wagombea wanaotaka kuwania nafasi hiyo kubwa kabisa, ambapo utaratibu wa ugawaji wa fomu hizo umeanza jana na utakamilika Julai 16 mwaka huu.
Akizungumza na wandishi wa habari baada ya kukabidhiwa fomu hiyo na Katibu Mkuu chma hicho, Renatus Muhabhi jijini Dar es Salaam jana, Dk. Malisema, alisema hatua yake hiyo haikutokana na msukumo wa kutaka madaraka bali imetokana na kuguswa umasikini wa Watanzania
Alisema, kuwa endapo chama chake kitamteua kuwa mgombea wanafasi hiyo na wananchi kumpa ridha hiyo atahakikisha anabadili mfumo wa utawala, ambao uongozi na usimamizi wa rasilimali za nchi zinasimamiwa na Watanzania wenyewe.
“Kuna wengi waliojitokeza na kuna vyama wapo wagombea wamefikia hadi 40 jambo ambalo linaweza kuwafanya wananchi wakajiuliza mbona wako wengi, kumbukeni Mwalimu Nyerere aliwahi kusema ikulu siyosehemu ya kukimbiliwa hivyo wananchi wanapaswa kufanya maamuzi mazuri wakati wa uchaguzi,”alisema.
Dk. Malisa, alisema nchi hii imeshikwa na watu wachache ambao wamekuwa wakiamua kuuza rasilimali za nchi bila ya kuwashirikisha wananchi, walipo hoji walipigwa mabomu.
Alisema kutokana na mazingira kama hayo anaamini kwamba kunahaja ya uongozi mpya na mwuelekeo mpya ambao utaweza kusimamia rasilimal, kwa ajili ya masilahi ya wananchi wote.
Dk. Malisa alisema kiongozi mzuri ni yule anayepigania masilahi ya wananchi lakini cha anashangazwa na kuona baadhi ya wagombea wa walioachia ngazi kwa ufisadi wamepewa fomu na vyama vyao huku wakitoa wakijitetea kwamba kila anayemtuhumu kwa ufisadi atowe ushahidi.
Alisema wakati umefika kwa Watanzamia kuwa na serikali waliyoichagua wenyewe kinyume na sasa.
“Nchi hii haiwezi kuondoka hapa ilipo kama Watanzania hawatauondoa uongozi huu uliyoko madarakani na kuirudisha Tanzania mikonomi mwa Watanzania kwa ajili ya kuamua mustakabali wao.
DK. Malisa, aliwahi kugombea ubunge mwaka 2010 kupitia chama cha TLP, katika jimbo la Moshi mjini, mkoani kilimanjaro.
Naye Katibu Mkuu wa Chama hicho, Muhabhi, awali alisema zoezi la ugawaji wa fomu za Wabunge na Madiwani unatarajiwa kuanza Julai 15 na utaendelea hadi Julai 22 mwaka huu.
Alitaja ada ya fomu ya mgombea urais kuwa ni sh 500,000, Mbunge sh. 100,000 na diwani sh. 50,000.


No comments:

Post a Comment