KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Friday 10 July 2015

POLISI TOENI UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA ZA UGAIDI

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP), Simon Siro.
BAADHI ya wakzi wa jiji la Dar es Salaam wameitaka serikali kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa zinazotolewa mara kwa mara n vyombo vya habari kwamba nchi hivi sasa inakabiliwa na tatizo la ugaidi.
Wakazi hao walisema hivyo baada ya hivi karibuni kusambaa kwa tarifa kuwa mkoani Morogoro kulitokea mapambano kati ya magaidi 50 na polisi.
Walisema wanaitaka serikali kupitia Jeshi la Polisi kufanya hivyo kwa vile wananchi hivi sasa wanaishi wakiwa na wasiwasi huku baadhi yao wamelazimika kuyama makazi yao kutokan na hofu ya kushambuliwa.
Hamisi Dihule, mkazi wa Mansese ambaye asili yake ni mkoani Morogoro, alisema ukimya wa serikali katika kulitolea ufafanuzi suala hilo kunawafanya wananchi washindwe kuelewa kuhusu ukweli taarifa hizo zinazozagaaa kila kukicha.
Alisema, ktika kuendeleza hofu kwa wananchi, juzi kuna taarifa kutoka mkoa wa Pwani ambazo zilithibitishwa na Kamanda wa Mkoa wa Pwani kwamba kuna kikundi cha magaidi kilitelekeza silaha baada ya mapambano na polisi.
Silaha zilizotelekezwa zilikuwa ni risasi 50 za shotgun, bomu moja lililotengenezwa kienyeji fulana tatu, kitabu kimoja cha kuruani, jambia moja na begi moja.
“Hiki kitu si cha kushabikia kwa sababu hata kuwatajataja magaini ni hatari na zaidi wapo wanaosema magaidi hao ni El Shabab,”alisema Dihule.
Dihule, alisema kitendo cha kukitaja kikundi hicho ambacho hakina mpango wa kushambulia nchi hii, kinaweza kuwajengea hasira na kikaamua kutekeleza mashambulizi kweli.
Sharifa Hamisi, alisema haamini kama watu hao wanaokamatwa kama kweli ni magaidi, bali anawachukulia watu hao kama wahalifu na vibaka tu.
Alisema hivyo, haingii akiakili kuwafanya watu hao waliokamatwa ktika maeneo ya mashamba huko wakafananishwa na magaidi, akibainisha kuwa wakati umefika kwa polisi kutoa taarifa kuhusu taarifa hizo na ikiwezkana kuwataka wanaotoa taarifa hizo kuacha kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment