Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia), akimkabidhi mfano wa kadi ya malipo ya
Tembo Card, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda za Nyanda za Juu
Kusini, Myriam Msalale (kushoto), itakayowawezesha
wagonjwa wanaofika katika hospitli hiyo kulipia huduma za matibabu kwa njia ya
kadi badala ya fedha taslimu. Uzinduzi huo ulifanyika mjini Mbeya mwishoni mwa
wiki. (Na Mpiga Picha Wetu)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (katikati), akiwa
katika picha ya pamoja na maofisa wa benki ya CRDB baada ya kuzindua huduma za malipo kwa njia ya kielektroniki katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda za Nyanda za
Juu Kusini mjini Mbeya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (katikati), akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda za Nyanda za
Juu Kusini baada ya kuzindua huduma za malipo kwa kutumia mfumo wa kielektroniki
badala ya fedha taslimu katika hospitali hiyo. Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa
Hospitali ya Rufaa ya Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Myriam Msalale.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akilipia huduma za matibabu kwa njia ya kielektroniki katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda za Nyanda za
Juu Kusini baada ya kuzindua huduma hizo. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Mbeya, Benson Mwakyusa, Kaimu Mkurugenzi wa
Hospitali ya Rufaa ya Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Myriam Msalale na Rahel Massawe.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Mbeya, Benson Mwakyusa (wa pili kulia) akiangalia risiti ya malipo baada ya Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei kulipia huduma za matibabu kwa njia ya kielektroniki wakati wa uzinduzi wa huduma hizo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda za Nyanda za
Juu Kusini, mjini Mbeya, mwishoni mwa wiki.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Hospitali ya Rufaa ya Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Myriam Msalale akimtembeza katika vitengo mbalimbali vya hospitali hiyo, Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Baadhi ya Mameneja wa Matawi ya Benki ya CRDB kutoka mkoani Mbeya wakiwa katika uzinduzi huo. Kulia ni Meneja wa tawi la Mbalizi, Chibby Chibby.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Mbeya, Benson Mwakyusa akizungumza katika uzinduzi huo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitari ya Rufaa ya Mbeya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa katika uzinduzi huo.
Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma za malipo kwa njia Kielektroni katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Huduma Mbadala za Benki wa CRDB, Joseph
Witts, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda za Nyanda za Juu
Kusini, Myriam Msalale.
Na Mwandishi Wetu, Mbeya
UONGOZI wa Hospital ya Rufaa ya Mbeya, imeingia makubaliano na benki ya CRDB ambapo sasa
wananchi watalipia huduma kupitia mfumo maalum wa kielektroniki kwa kadi za
benki hiyo badala ya fedha taslimu.
Akizungumza
kwenye hafla fupi ya kuzindua huduma hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo,
Myriam Msalala, alisema kuwa huduma hiyo itaisaidia hospitali hiyo kuongeza
makusanyo ya fedha.
Alisema kuwa
awali kabla ya kuanza kutumia mfumo huo,
hospitali hiyo ilikuwa ikikusanya kiasi cha Sh. Milioni 38 kwa mwezi na kwa
sasa wanakusanya milioni 50.
“Kwa kweli
tunawashukuru sana CRDB, kwa sasa hakuna mianya ya upotevu wa fedha kwa kuwa
hatutumii tena mfumo wa malipo ya fedha taslimu, tunakusanya kupitia kadi za
benki,” alisema Myriam.
Alisema kuwa
hakuna mwananchi ambaye atakubaliwa kulipia kwa fedha taslimu na badala yake
wanapewa elimu ya kutumia mfumo huo wa kadi za benki.
“Wagonjwa
wanaokuja hapa, watakuwa na kadi za benki ambapo baada ya kupatiwa huduma watatoa
kadi kw wahuduma wetu au wakala na tutakata malipo hayo,” aliongeza kusema
Myriam.
Kwa upande
wake, Mkurugenzi wa CRDB, Dk Charles Kimei, alisema kuwa benki hiyo tayari
imeingia makubaliano na hospitali zaidi ya 20 ikiwemo Hospitali ya taifa ya
Muhimbil kwa ajili ya huduma hiyo.
“Huu ni
mfumo salama, na tayari tupo kwenye mazungumzo na hospitali nyingine kubwa ili
kujiunga katika mfumo huu, kwa sasa tayari hospitali 20 tumekshakubaliana
nazo,” alisema Kimei.
Alisema
mfumo huo utarahisisha huduma za hospitalini na kupiunguza gharama za
uwendeshajiwa hospitali.
Uzinduzi huo
wa mfumo mpya wa malipo ulishuhudiwa na
wakurugenzi na wafanyakazi wa CRDB na wafanyakazi wa hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment