KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Thursday 20 August 2015

MAKONDA AWASHUKIA WABADHIRIFU WA MALI YA UMMA

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Paul Makonda, amsema Kamati ya Wataalamu aliyounda hivi karibuni ili kuchunguza kuharibika kwa barabara mpya za lami, imebaini kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu za kiufundi.
Alisema hivyo baada ya kubaini barabara zilizojengwa kushindwa kudumu kwa muda uliotarajiwa na hivyo kuzua malalamiko kutoka kwa watumiaji na walipa kodi kwa ujumla.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini jana, Makonda, alisema Manispaa ya Kinondoni ni wilaya yeneye mtandao mkubwa wa barabara za lami kuliko wilaya zote 166 Tanzania Bara.
“Manispaa ya Kinondoni ina barabara za lami zenye urefu wa kilometa 241.1 ambazo ni sawana asilimia 22 ya barabara za lami katika halmashauri zote (kilometa 1,117.5),”alisema Makonda.
Alisema, ukiukwaji huo ulijitokeza katika ushahidi wa kuonesha kuwa makablasha ya zabuni yalithibitishwa na Bodi ya Zabuni, hakukuwa na makadirio ya kihandisi ya thamani ya kazi.
Aidha, Makonda, alisema katika maeneo mengine haukufanyika usanifu na pia hakukuwa na michoro ya kihandisi kwa barabara zote.
“Maelezo ya kazi kwenye jedwali la bei hayakuwa na uhusiano na viwango vya kazi husika,”alisema Makonda.
Makonda alisema baada ya kupokea ripoti hiyo, atakutana na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ili kuona ni hatua gani zitakazochukuliwa kwa watendaji wote waliohusika katika ujenzi wa barabara hizo kwa kiwango cha chini.

“Watakaobainika katika ubadhilifu huo itabidi wafukuzwe kazi kazi na kama atashindwa kuwafukuza basi kunaulazima wa kufanyakazi kwa waliowateua wahusika,”alisema Makonda.

No comments:

Post a Comment