KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Monday 17 August 2015

MKONGO AIOMBA SERIKALI YA TANZANIA KUMSAIDIA KTIKA KESI YAKE YA KUIBIWA MADINI

RAIA wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Ally Kamile, ameiomba Serikali ya Tanzani kumsaidia katika kesi yake ya kuibiwa madini yenye thamani ya sh milioni 156 na Watanzania wakishirikiana na raia wenzake wa wanaoishi nchini.
Kamile aliomba msaada huo kutokana na Malalamiko kuhusu kukaliwa kwa kesi ya jinai Namba Maag/IR/7196/2013 aliyofungua katika Kituo cha Polisi Magomeni mwaka 2013, kuchukua muda mrefu bila ya kupatiwa ufumbuzi katika.
Hayo aliyasema jijini Dar es Salaam leo,wakati alipozungumza na mwandishi juu ya mateso aliyoyapata kipindi chote alichofuatilia haki yake, ambapo katika wizi huo pia aliibiwa vitu vingine pia.
“Mali nyingine zilizoibiwa baada ya kunyweshwa sumu ni compyuta mpakato simu mbili za mkononi na begi mbili za nguo na cha kushangaza watuhumiwa hawakuchukuwa fedha nilizo kuwa nazo mfukoni kiasi cha dola za kimarekani 500,”alisema Kamile.
Kamile, alisema hivyo kwa vile watuhumiwa waliohusika katika tukio hilo la kumnywesha dawa za kulevya kisha kumuibia wanafahamika lakini cha kushangaza hadi leo hawajachukuliwa hatua za kisheria.
“Inasikitisha kuona polisi wa kituo hicho kushindwa kunitendea haki na baadala yake, wakishirikiana na watuhumiwa ambao majina  yao wanayo walinizushia makosa ya kutishia kuua kitendo kilichonifanya Machi mwaka huu ni hukumiwe miezi sita gerezani,”alisema Kamile.
Kamile, alisema alijengewa mazingira hayo ya kufungwa baada ya kukwenda kuomba msaada ya katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).
Alisema kuwa Ofisi hiyo ya DPP, ilimkabidhi barua ailiyosainiwa na  Matendo Manono kwa niaba ya Mwanasheria wa Serikali Mfawadhi, ambayo ilimuelekeza kurudi kwa Mkuu wa Upelelezi Kinondoni ili kuweza kupata msaada kuhusu kesi hiyo.
“Barua hiyo iliandikwa Otoba 27 mwaka jana, ikiwa na kicha cha habari kinachosema yahusu Malalamiko kuhusu kukaliwa kwa kesi ya jinai Namba Maag/IR/7196/2013 iliyofunguliwa katika kituo cha Polisi Magomeni,”alisema Kamile.
Kimile, alisema baada ya kutoka gerezani kwa msamaha wa Rais Jakaya Kikwete, aliyoutoa hivi karibuni, alikuwa akiogopa kurudi kituo cha polisi Magomeni, hadi alipopatiwa ushauri na gazeti hili kuwa aende kwenye Ofisi ya Upelelezi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni.
Hata hivyo, Kamile, alisema wabaya wake bado wanaendelea kushirikiana na polisi hao wa Magomeni kumtishia kwa kumfikisha mahakamani lengo likiwa aogope kufuatilia haki yake. 
Alimtaja mapelezi  aliyekuwa akishugulikia suala hilo kwa jina moja la Denis ambaye alidai kuwafahamu watuhumiwa hao ambao majina yao (tunayo).
Hata hivyo, alipotafutwa Denis ili kutoa ufafanuzi kuhusu madai hayo, alisema kuwa hahusiki na suala hilo akibainisha kuwa wako wanaohusika watafutwe.

No comments:

Post a Comment