ZAIDI yawanachama 500 wa Wakala Forodha (TAFFA),
wamesema watagoma kutoa huduma nchi nzima endapo serikali itashindwa kuondoa
dhamana ya sh. milioni 100 ambazo ni kwa ajili ya kuhuisha leseni za uwakala wa
forodha mwaka 2016.
Kwenye gazeti la serikali Julai 22 mwaka huu linawanyima
uhuru katika soko la ushindani la Afrika Mashariki.
“Madhara yatakayotokana na amri ya TRA yakuweka sh.
milioni 100; ni kampuni nyingi za kitanzania zitakufa, familia nyingi Tanzania
nzima zitaumia kutokana na ajira zao kupotea na itajengeka chuki kati wananchi
na serikali,”alisema Ngatunga.
Alisema nia ya kukutana na serikali kuu kutaka
kusikilizwa kilio chao kuhusu dhamana hiyo, kwani kuna upungufu mwingi
unaotekelezwa na TRA ambao wataifahamisha serikali katika kikao hicho
wanachoomba.
Ngatunga, alisema tangu kuanza jambo hilo Novemba
mwaka jana wamefanya jitihada za kuonana na Waziri wa Fedha na Uchumi Saada
Salumu Mkuya lakini bila mafanikio.
Alisema miongoni mwa majibu waliyopewa na TRA kwa
mdomo: Biashara ni mchezo kama michezo mingine, anayeweza kucheza acheze,
asiyeweza mchezo, mchezo utakuwa umemshinda.
“Tunaiagiza Wizara ya Fedha na Uchumi kuondoa agizo
lao la kuweka sh. milioni 100 mara moja, ili kuweza kuimarisha umoja na
mshikamano wa kitaifa na kuiagiza TRA kuondoa fikra za kibaguzi kwa Watanzania.
No comments:
Post a Comment