DIWANI wa Kata ya Saranga Kimara jijini Dar es Salaam , Ephraim Kinyafu, amesema hadi sasa Shirika la Maji Safi na Majitaka (Dawasa),imeweka
alama ya ‘X’nyumba 15 Matangini, nyumba 50 Stop Over na bado wanaendelea kuweka
alama nyumba nyingine kwa ajili ya ubomoaji.
Kauli ya Kinyafu imekuja siku moja baada ya wananchi wa Kimara
Matangini kulalamikia kitendo cha Shirika la majisafi na
majitaka(Dawasa) kuwataka wabomoe nyumba zao kwa madai kuwa wamejenga
juu ya bomba la maji na wasipofanya hivyo ikiwabomolea watalipa gharama.
Akizungumza na jijini leo, Kinyafu alisema nyumba hizo zimebainika kuwa
zimejengwa kimakosa lakini pia ameshangazwa na nyumba nyingine ambazo
zimewekewa alama ya ‘X’ ambazo
zipo umbali wa mita 7.5 toka
katikati ya bomba hilo.
“Upimaji wa upana halisi haujazingatiwa kuna maeneo wamepima zaidi
ya mita tano,mita 9 mpaka 14”.alisema Kinyafu.
Alisema sheria ya mwaka 1964 inasema upana halisi toka bomba hilo inatakiwa kuwa mita
tano lakini anashangaa Dawasa walishaweka alama katika nyumba nyingine ambazo
zipo nje ya mita tano nyumba hizo zipo
umbali wa mita 7.5, mita 9 na nyingine
mita 14.
Kinyafu alisema tangu wananchi hao wapewe amri ya kubomoa,
wananchi zaidi ya 30 hawana makazi ya kuishi.
“Kuna mwanamke mmoja ambaye jina lake silifahamu
anawatoto saba na wajukuu hana mahali pa kuishi na hivi sasa amehifadhiwa na
jirani”alisema Kinyafu.
Kinyafu alisema ameongea na
Dawasa wakishirikiana na Dawasco waongeze muda ili wananchi wapate nafasi ya
kuhamisha mali
zao na sio kutaka wavunje haraka kwani
watapata athari kwa kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment