TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII AFRIKA MASHARIKI NA KATI (ECASSA)
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania, (TSSA), Meshack
Bandawe, (katikati), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari
kwenye ukumbi wa idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Februari
14, 2016. Pamoja na mambo mengine Bandawqe alisema, mkutano wa mwaka wa
Muungano wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Mamlaka za Usimamizi Sekta za
Hifadhi za Jamii kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (ECASSA),
utafanyika nchini kuanzia Februari 18mwaka huu 2016. (Kushoto) ni Naibu
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Vincent Tiganya, na kulia ni
mjumbe wa kamati ya waandaaji wa mkutano, Rehema Kabongo.
…………………………………………………………………………………………………………
MAKAMU wa Rais Samia Suluhu
Hassani anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa muungano wa mifuko ya
hifadhi ya jamii(Pensheni na afya), mamlaka ya usimamizi za hifadhi ya jamii
za nchi za Afrika mashariki na kati (ECASSA).
Nchi wanachama watakaoshiriki katika mkutano huo ni Kenya, Uganda,
Rwanda, Burundi, Tanzania, Zambia na Sudani ya Kusini.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo, Katibu
wa Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania(TSSA), Meshack Bandawe alisema ,
dhumuni la mkutano huo ni kujadili sera zinazohusiana na sekta ya jamii.
Alisema mkutano huo utafanyika Februali 18-19 mwaka huu katika
ukumbi wa Benki kuu(BOT) ambapo siku ya kwanza washiriki watapokea mada
mbalimbali za kitaalamu kuzijadili na kutoa mapendekezo yao.
“Siku ya pili itakuwa maalumu kwa mawaziri kuzungumzia hatua
zinazochukuliwa nan chi zao ku[punguza tatizo la ajira. Inapendekezwa kwa
upande wa Tanzania itolewe na waziri mmoja kuonyesha hatua za kisera na mipango
zinazochukuliwa kukuza ajira na kuboresha hifadhi ya jamii ili kuchangia upunguzaji
wa hifadhi.
Alisema mkutano huo pia utapokea mada zilizowasilishwa na
wataalamu ambapo zitachambuliwa na kuweka maadhimio kwa ajili ya kuboresha
sekta ya hifadhi ya jamii katika nchi wanachama.
“Kwa mara ya kwanza mkutano kama huu ulifanyika mjini mwanza mwaka
2010 na mwaka huu Tanzania inakuwa mwenyeji katika mkutano huo,”alisema.
Alisema kauli mbiu ya mkutano huo ni ‘kuainisha sera za kiuchumi,
upatikanaji wa ajira na maendeleo ya sekta ya hifadhi ya jamii katika Afrika Mashariki na
kati’.
Aidha alisema washiriki wa mkutano huo watakuwa Mawaziri wa sekta
zenye dhamana katika mifuko ya hifadhi ya jamii(Pensheni, bima ya afya na fidia
kwa wafanyakazi).
“Pamoja na mawaziri hao
watakuwepo makatibu wakuu wa Wizara na wajumbe wa bodi za mifuko mifuko hiyo,”alisema.
Muungano wa mifuko ya hifadhi ya jamii Pensheni na afya na mamlaka
za usimamizi za hifadhi za jamii za nchi
za afrika mashariki na kati hadi sasa taasisi 23 zinazounda umoja huo.
No comments:
Post a Comment