WAFANYABIASHARA wa Soko la Yombo Makangarawe wamesema kuwa wamejipanga kuliboresha Soko lao huku wakiwataka viongozi wa Kata hiyo kuhakikisha wanashawishi madalali kuleta magari ya bidhaa Sokoni hapo Kwa ajili ya kumwaga kama ilivyo katika masoko ya Temeke Stereo.
Walisema hayobaada ya kukamilika ujenzi wa Soko
hilo ambapo kwa muda mrefu kulikuwa hakuna Soko hivyo ujio wa Soko hilo ambalo
lilifunguliwa hivi karibuni na kiongozi wa mbio za Mwenge mwaka 2015 kumefanya
watu wa Makangarawe kuwa na Soko lao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana,
kwaniaba ya wananchi wake Diwani wa Makangarawe (Chadema), Dk. Idd
Mahuta alisema kuwa mbali na kuwepo kwa Soko hilo bado uendeshaji wake
umekuwa mgumu kutokana na wanchi kukimbilia masoko ya mbali na kuliacha
Soko hilo likikosa wateja.
“Kitokana na
matatizo hayo tumeamua kuhamasisha wafanyabiashara hao kila aliyepewa kizimba
kuhakikisha anafanya biashara hapa,”alisema Mahuta.
Alisema, kuwa matatizo makubwa katika soko hilo
ni kwamba watu walikamata vizimba lakini cha kushangaza hawafanyi biashara
sasa ni wakati muafaka kwa kila mfanyabiashara anaendelezaji sehemu
yake.
"Tunawataka wafanyabiashara wetu kufanya
biashara hapa na sisi kama viongozi tutaendelea kufanya jitihada za kuhamasisha
watu kuja katika Soko hili kwani eneo linauwezo wa kubeba wafanyabiashara 800
hadi 900,”alisema Dk. Mahuta
Aidha akizungumzia uwezo wa soko hilo Dk. Mahuta,
alisema lina uwezo wa kulisha katika maeneo ya Buza hadi Yombo kilakala hivyo
kuna haja ya kuliboresha soko hilo ili liweze kukidhi haja.
Pia aliwataka wananchi wote wanaozunguka eneo hilo
kuhakikisha wanalitumia Soko hilo ipasavyo kwa ajili ya kuboresha vipato vyao
na kipato cha Halmashauri ya Temeke.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Dovyo,
Bruce Mbagwile, alisema kata hiyo inamitaa mitano ambapo kimsingi mitaa yote
hiyo inategemea Soko hilo
Aidha, alisema kuwa walichokifanya wananchi hao
ni kurudisha muamko kwa wafanyabiashara hao ili kila mmoja aliyechukua kizimba
anafanya biashara na si vinginevyo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment