BAADHI ya abiria wanaotumia usafiri wa mradi wa mabasi
yaendayo haraka, wamesikititishwa na ucheleweshaji wa uzwaji wa kadi za
kutunzia nauli kila wanapotaka kusafiri katika mabasi hayo.
Baada ya uzinduzi wa mabasi hayo Mei 10 mwaka huu, abiria
hao waliahidiwa na maofisa waliyoko kwenye vituo vya mabasi hayo kwa ajili ya
kutoa elimu kuhusu atumizi ya magari hayo, kwamba wangeanza kuuziwa kadi hizo
kuanzia Mei 12 mwaka huu.
Wakizungumza jijini Dar es Salaam jana, Abiria hao, walisema
walifika katika vituo hivyo asubuhi ili kujipatia kadi hizo lakini wakazikosa
kwa madai kuwa bado utaratibu wake unaandaliwa.
Dorcas James, alisema wamefikia hatua hiyo kwa vile
wanaamini kumiliki kadi hiyo kutaondoa usumbufu kwa abiria anayetaka kusafiri, kwani atakapofika kituoni hatapanga foleni ya
kununua tiketi.
Hata hivyo, alisema kuchelewa kuuzwa kwa kadi hizo kuna tiashaka
kwami maofisa waliyokuwa katika baadhi ya vituo hivyo walishindwa kutowa majibu
ya kuridhisha kwa abiria kuhusu kuchelewa huko.
“Unajua kuchelewa kuuzwa kwa kadi hizo kunaonesha jinsi waendeshaji
wa mradi huo walivyokuwa hawajajiandaa kuanza kwake,”alisema Dorcas.
Alisema, pamoja na kuwepo utaratibu mfumo mwingine wa
tiketi, anaamini siku ya Mei 16 mwaka huu utakapoanza utaratibu wa malipo
kutakuwa na vurugu kutokana na wingi wa abiria watakaokusanyika kwa ajili ya
kusafiri.
Naye James Charles, alisema mwiitikio wa abiria ni mkubwa
kwa hivyo utoaji wa tiketi kwa siku hiyo hiyo ya safari utaleta usumbufu kwani
unaweza hata kuchelewesha safari.
“Kingine magari bado hayaoneshi ruti hivyo wakati mwingine
kuwafanya abiria kupanda gari lolote na kujikuta akianza kuhangaika mara
anapojikuta amejaribu kuingia kwenye gari ambalo siyo lake,”alisema Charles.
Kwa nyakati tofauti mofisa waliyoko kwenye vituo bila
kutaja majina yao walisema awali walitoa ahadi hiyo ya kuanza kuuzwa kadi hizo
kutokana na maaelekezo ya viongozi wao.
Walisema, baada ya kukwama kuuzwa kuanzia juzi, viongozi
wao wamesema wanalishugulikia na kuanzia sasa zitaanza kuuzwa.
No comments:
Post a Comment