WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI, WILLIAM LUKUVI |
SERIKALI
imepiga marufuku matumizi ya Ramani ya Tanzania baada ya kubaini upotoshwaji wa
mipaka ya nchi jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa nchi.
Hatua hiyo
inakuja baada ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kubaini
matumizi ya ramani ya Tanzania kwenye majarida, magazeti na hata luninga
inayopotosha mpaka kwamba sehemu ya ziwa Nyasa ikionesha kuwa mpaka wake unapita
pembezoni mwa ziwa.
Katika
mazungumzo yake na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa
Upimaji na Ramani, Justo Lyamuya, alisema ili kuepusha upotoshaji huo wa mipaka
ya nchi serikali inashauri kwamba kila mmoja lazima atumie ramani sahihi.
Alisema,
kuwa kitendo chochote cha kuchapisha ramani yenye makosa kwa makusudi au bila
kujua kwa kutumia vyanzo visivyo rasmi ni kosa kwa mujibu wa sheria za nchi
hivyo atakaye kaidi baada ya kuelimishwa anaweza kuchukuliwa hatua.
Lyamuya, aliwataka
watumiaji wa ramani kutambuwa kuwa ramani sahihi ya Tanzania inatakiwa kuonesha
mpaka kwa sehemu ya maziwa ya Victoria, Tanganyika na Nyasa ukipita katikati ya
maziwa hayo na siyo vinginevyo.
Aidha, wadau
wote wanapaswa kutambua kuwa Idara ya Upimaji na Ramani ndiyo yenye mamlaka ya
kuandaa, kuchapisha, kutunza na kusambaza ramani zote nchini, ambayo ipo tayari
kutoa ramani kwa matumizi yaliyokusudiwa ikiwa ni pamoja na kutoa elimu na
ushauri kuhusu usahihi wa ramani kabla ya kuitumia.
“Kutumia vyanzo visivyo rasmi ni kosa kwa
mujibu wa mamlaka (Instrumen) ya Waziri aliyepewa dhamana ya kusimamia sekta ya
aardhi ikiwemo masuala ya upimaji ramani,
“Jambo hili
likiachwa liendelee kuna hatari nchi ikaingia kwenye mgogoro kwani kuna baadhi
ya nchi zimeingia kwenye migogoro chanzo ikiwa na kugombea mipaka,”alisema Lyamuya.
“Napenda kuchukuwa fursa hii kuwatangazia
Watanzania na wadau wote hapa nchini kuwa ramani sahihi ya Tanzania inayoonesha
mpaka wa Tanzania ni hii ambayo kwa sehemu ya ziwa Nyasa mpaka wake unapita
katikati ya ziwa hilo,”alisema Lyamuya.
Hata hivyo,
Lyamuya, alisema kwa yeyote nahitaji ramani hiyo sahihi kwa ajili ya matumizi
afike katika duka la wizara hiyo lililoko Temeke, mahali palipokuwa Makao Makuu
ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Alisema, vile vile ramani hiyo pia inapatikana katika
tovuti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa anwani;www.ardhi.go.tz
Akizungumzia uasalama wa mipaka ya iliyoko baharini,
Lyamuya, alisema hadi sasa mipaka yote haina matatizo nchi zote zinazopakana na
Tanzania zinaheshimu makubaliano saini.
No comments:
Post a Comment