KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Tuesday 17 May 2016

KANISA LA EAGT LA MTAMBULISHA ASKOFU BROWN MWAKIPESILE




ASKOFU Mkuu wa Kanisa  la The Evangelistic Assemblies of God   Tanzania (EAGT), Dk Brown  Mwakipesile  amewataka wa umini wa kanisa hilo kudumisha amani, ambayo itawafanya waweze kuendesha ibada katika hali ya mshikamano.
Hayo aliyasema juzi, wakati  alipoongoza viongozi na washirika wa makanisa ya EAGT katika ibada maalum ya kumtambulisha kwa wa umini, iliyofanyika katika Ukumbi wa PTA uliopo kwenye viwanja vya maonesho ya Kimataifa ya biashara ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Askofu Dk. Mwakipesile alishika nafasi hiyo Oktoba mwaka jana baada ya Agosti  29   2013, kufariki Mkuu wa Kanisa hilo, Askofu Dk. Moses Kulola.
Ibada hiyo ilihudhuriwa, baadhi ya viongozi  na washirika wa makanisa ya EAGT kutoka majimbo ya Kinondoni, Temeke na Pwani, ambapo Dk.Mwakipesile aliwataka waumini wa kanisa hilo kuwa na moyo wa kujitolea kwa ajli ya  kununua viwanja vya kujenga makanis
Alisema makanisa yakiongezwa na waumini wakishiriki katika ibada wataweza kujua mahitaji yao makubwa ambayo yanahitajika kupatiwa ufumbuzi wa pamoja ikiwa ni kati ya viongozi na waumini.
“Watu wasome,wazalishe ili kizazi kinachokuja kiweze kufundishwa Injili, tukitaka tushinde lazima tuhubiri Injili,”alisema Askofu Mwakipasile nakuongeza;
“Mimi wakati nachaguliwa sikuwa na wazo la kuchaguliwa, tangu nimeanza kumtumikia mungu nimeanza uongozi ngazi za chini,kitu ambacho nimeweza kujifunza kwa marehemu Kulola ni kujiuliza wapo wangapi wenye mfano kama wake yeye mwenye uchungu nikabaki tuu kumuombea hivyo basi  nawasisitiza tuitangazeni Injili,”alisema Dk. Mwakipasile.

No comments:

Post a Comment