WAKAZI wa Kitongoji cha Tembo, Hondogo Kata ya Kibamba
wilayani Kinondoni, wamesema wanatarajia kutumia nguvu ya umma kubomoa banda
lililojengwa na kuziba barabara katika eneo hilo.
Mgogoro huo wa kuzibw barabara hiyo kunawafanya wakazi wa
eneo hilo kupata tabu katika kujipatia huduma za kijamii upande wa pili.
Wakizungumza na SAUTI YA WALEMAVU.BLOG leo, wakazi hao walisema hawaelewe
kuna kitu gani kinachowafanya viongozi wa kuanzia ngazi ya mtaa, Kata hadi Manspaa
washindwe kumuondoa mvamizi huyo.
Kwa niaba yao, Ramadhan Mkude, alisema wanatarajia kufanya hivyo kwa vile mgogoro huo
umechukuwa muda mrefu, bila viongozi wa Manispaa hiyo kuchukuwa hatua ya
kuumaliza japo wanaufahamu vizuri.
“Sasa acha tujipange kwa ajili ya kulibomoa wenyewe ili
kuondoa usumbufu tunaoupata kutokana na kuzibwa barabara, hatupendi kutumia
nguvu lakini wakati mwingine haki inawezekana ikaja kwa njia hii,”alisema
Mkude.
Mkude, alisema mgogoro huo una zaidi ya miaka mitano sasa
ambapo Mei 13, 2013, baadhi ya viongozi wa Idara ya Ardhi walitembelea eneo
hilo ili kufanya uchunguzi wa mgogoro huo.
Alisema walichobaini katika ziara hiyo ni kwamba Ramani
inaonesha kuwa barabara inayolalamikiwa inaupana wa mita kumi kutoka barabara
itokayo Morogoro kuelekea Kibwegere.
Mkude alisema katika taarifa ya uchunguzi huo walibaini kuwa
ni kweli kuna banda limejengwa kinyume cha sheria katika barabara hiyo, huku
mmiliki akidai kuwa hilo ni eneo lake.
Alisema hata hivyo, katika taarifa hiyo wamejiridhisha
kuwa mmiliki anayedai kuwa eneo hilo ni lake anaonesha kuwa mbishi kwani pamoja
na kutakiwa na Baraza la Ardhi kufika katika kikao siku hiyo, alikaidi wito huo
halali.
Mkude alisema baada ya uchunguzi huo Ofisi ya Mkurugenzi
wa Maniaspaa hiyo ya Kinondoni, Oktoba 25, 2013, ili mwandkia barua Afisa Mtendaji
Kata wa Kibamba, barua hiyo ikisainiwa
kwa niaba ya Mkurugenzi na Ofisa aliyeitwa Omary Mauya.
Alisema barua hiyo, ilisema kwa kuwa barabara hiyo iko
chini ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni hivyo basi ikamuomba kupitia
ofisi yake ya Kata afanye utaratibu wa kubomoa banda hilo ili barabara hiyo
iweze kupitika na kuondoa usumbufu kwa wananchi hao.
Mkude, alisema lakini hadi leo banda hilo lipo, mmiliki
wake anazidi kero kwani wakati mwingine
anaingilia miundombinu ya maji hivyo kuwafanya wananchi wataabike katika kupata
huduma hiyo.
No comments:
Post a Comment