KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Tuesday 21 April 2015

ATME YAUNGA MKONO SERIKALI KATIKA KUFUTA USAJILI WA TAASISI



KATIBU wa shirika la Dawa  Asili na Ulinzi wa Mazingira nchini Bonivetura Mwalongo ameunga mkono Tamko la Serikali la kutaka kufuta usajili wa baadhi ya Taasisi na Mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yalisajiliwa kuazia mwaka 1954 hadi 2013 kutokana na kushindwa kufuata sheria na masharti ya usajili.

Akizungumza Ofisini kwake Dar es Salaam jana mbele ya waandishi  wa habari waliofika ofisini hapo kutaka kujua kwanini Chama cha Watatibu wa Tiba Asili Tanzania (ATME) kimefutwa rasim na kuazishwa kwa Chama kingine cha Shirika la Dawa Asili na Ulinzi wa mazingira.

Mwalongo alisema kuwa Chama hicho kilipoteza sifa za kuendelea kuwa uhai ,hivyo kufa kwake kumekwenda sambamba na Tamko la Serikali la kutaka kufuata taasisi na mshirika  yote ambayo yamepoteza sifa na masharti ya usajili wake,hivyo hata ATME ilipoteza sifa hizo.

Alisema kuwa lazima ifike wakati watanzania waache kuchochea hata mambo ambayo yapo kisheria badala yake waisaidie Serikali katika kusimamia sheria ziliwekwa,hivyo hata viongozi wadini wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha watu hawavunji sheria na si wao kuwa sehemu ya walalamikaji.

Alisema kuwa viongozi wa dini wao ni dira katika nchi, hivyo hategemei kuona kunajitokeza hali yeyote ya vurugu na lazima ielewekwe kwamba viongozi hao wanamchango mkubwa katika taifa hivyo anaamini Serikali haitatumia mabavu katika hilo bali kila jambo litafuata sheria zilizowekwa.

“Lazima sheria ifuatwe kwani hatuwezi kuwa na taifa ambalo watu wake hawafuati sheria zilizokwa ,hivyo naunga mkono tamko hilo la Serikali na kamwe lisitafasiliwe vibaya na hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu,”alisema Mwalongo.

Aliongeza kuwa tatizo kubwa lililopo hivi sasa katika nchi yetu watanzania wanapenda kuchanganyika mambo ya kisheria na siasa hivyo lazima siasa ikae mbali na hasa linapokuja suala la kisheria.
Katika hatua nyingine akizungumzia shirika hilo jipya alisema kuwa alisema kuwa lipo kwa ajili ya kuendelea kufanya kazi ya kusimamia wadau wa Dawa za Asili nchini ili waweze kufanya kazi kwa kufuata miongozo mbalimbali kwa mujibu wa sheria zilizokwa.

Mapema mwezi huu Serikali kupitia Wizara ya mambo ya ndani ya nchi ili tangaza kufuata taasisi na mashirika yote ikiwamo taasisi za dini  baada ya kubainika kuvunja sheria ikiwemo kushindwa kupeleka taariza za ukaguzi wa hesabu zao katika kila mwaka.

No comments:

Post a Comment