BARAZA la Wanawake la Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Bawacha), Jimbo la Ukonga, limetoa msaada wa vyakula kwa vikongwe na
wajane ambao wanahitaji kusaidiwa kwa hali na mali kutokana mazingira magumu
wanayoishi.
Akizugumza wakati wa makabidhiano hayo
yaliyofanyika Mtaa wa Kiyombo Kata ya Kitunda wilayani Ilala jijini Dar es
Salaam, Katibu wa Bawacha Asia Msangi, ambaye ndiye mfadhili mkuu wa misaada
hiyo, alisema kuwa vikongwe na wajane ni kundi ambalo serikali imelisahau
kitendo ambacho kinawafanya wajisikie kama vile hawana haki ya kuishi katika
nchi yao.
Alisema Bawacha, limefikia hatua hiyo, baada ya
kubaini miongoni mwa watu hao wamo walioshindwa kupata huduma mbalimbali za
kijamii ikiwemo watoto wa familia hizo kukosa elimu.
“Kwa mfano kundi hili la vikongwe, hawa ni watu
ambao wamelitumikia taifa kwa uadilifu wakati wa tumishi wao sasa sio vizuri
kwa serikali ikawasahu,”alisema.
Asia, alisema Chadema ni chama makini,
akibainisha kuwa utoaji huo wa misaada haukuanza mwaka huu bali ni mwendelezo
nadni ya kipndichote cha miaka mitano.
Aliyekuwa Katibu wa Jimbo hilo Juma Mwipopo,
aliweleza vikongo na wajane hao kuwa matatizo yao yametokana na serikali ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambayo viongozi wake wameweka ubinafsi mbele.
Alisema kama wananchi wanahitaji mabadiliko ni
vema wakaiondoa CCM katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanika Oktoba mwaka
huu.
“Wazee wangu tambueni kuwa fedha zipo zinatengwa
na zinaletwa katika kata yenu, lakini uchoyo na kukosa uadilifu kwa viongozi
waliyoko madarakani kutojali watu wenye mahitaji maalum hali inayoifanya nchi
ionekane haipendi kundi hilo,”alisema Mwipopo.
Mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Staf
Sajent Machael Marwa, alisema wanakishukuru Chadema kwa kuwapatia msaada huo
kwa vile haujatokea kwa vikongwe wa kata hiyo kupewa misada.
“Huu msaada ni mkubwa kwa kuwa wako vigogo
wameshindwa kufanya hivyo katika maisha yao sasa kwani sisi tusishukuru
tunawomba wengine nao wapige mfano kama huu wa Chadema.
Naye Wegesa Borogo, amabye ni mjane alisema kuwa
wanakiomba chama hicho kuharakisha mpango wake wa kuanzishia Saccos kwani
anaamini itawasaidia katika kujiletea maendeleo katika familia zao.
No comments:
Post a Comment