KAMANDA wa Kikosi cha Usalama
Barabarani Mohamed Mpinga, ametoa onyo kwamba Jeshi la Polisi nchini halitasita
kuwakamata watu wanaotoa taarifa za ajali za uongo katika mitandao ya kijamii wakionyesha
aina ya basi na kudai kuwa yamepata ajali.
Mpinga, alitoa kauli hiyo
wakati alipozungumza na wandishi wa habari, kuhusu malalamiko kutoka Kampuni ya
Dar Express kwamba katika kipindi cha wiki mabasi ya kampuni hiyo yamehusishwa mara
nne kwenye mitandao ya kijamii kuwa yamepata ajali huku taarifa hizo si za
kweli.
Alisema, baada yakupokea
taarifa hizo za uzushi, tayari wamekwishaanza uchunguzi ili kuwabaini watu hao
ambao hadi hivi sasa haileweki wana lengo gani.
“Ni kweli picha za ajali za
mabasi ya Dar Express zilikuwepo zilionekana kweye mitandao ya kijamii hali
iliyofanya wananchi kutoka pembe zote za nchi,”alisema.
Mpinga, alisema vitendo
vinavyofanywa na watu hao ni ukiukwaji wa sheria kwa vile wanajua fika kuwa
hakuna gari la kampuni hiyo lililopata ajali.
Alisema watu hao katika
kutekeleza uzembe wao wamekuwa wakiweka katika mitandao picha za mabasi ambayo
yalipata ajali niaka sita iliyopita.
“Hii ni hatari wamekuwa
wakizusha hofu katika familia za jamaa ambao walikuwa ndugu zao wako safarini
na wapo watu waliokumbwa na shinikizo la damu kutokana na taarifa hizo ni
waombe watanzania kuwa waitumie mitandao hiyo kwa lengo la kujielimisha,”alisema.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Dar Express,
Yudika Mremi, amewaomba radhi abiria wake na kwamba hakuna basi la kampuni hiyo
lililopata ajali hivi karibuni.
Alisema kutokana na taarifa
hizo, uongozi wa kampuni hiyo tayari umekwishatoa taarifa polisi, ili wafanye
uchunguzi wao na hatmaye kubaini malengo ya watu wanaotoa za upotoshaji.
Mremi, ameitaka jamii kutoa
ushirikiano katika kuwasaka watu hao ambao katika nia yao
ningine ni kuvuruga biashara za wafanyabiashara wengine jambo ambalo
halitawaletea manufaa katika maisha yao.
No comments:
Post a Comment