Kundi la wanachama wa Chadema, ambao wamejitokeza kwa pamoja kutangaza nia ya kugombea Ubunge na Udiwani katika Jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam, leo |
Jimbo hilo ambalo lina Kata 13 linaongozwa na Naibu
Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Idadi ya watia nia ya Ubunge wako 20
ambao miongoni mwao wanawake ni wanne, huku wale wa udiwani wako 50 kati ya hao
wanawake 10.
Akizungumza
na waandishi wahabari, leo jijini Dar
es Salaam, alisema
watia nia wote wameamua kukutana, kutangaza nia ya Ubunge na Udiwani kwa pamoja ikiwa ni ishara ya kuweka tofauti
zao pembeni.
“Watia nia wote ni wasomi na wanakubalika nje na ndani ya chama chetu, kauli yetu ni kuruhusu Demokrasia ichukue nafasi kwani tunajua nafasi iliopo ni moja tu, hivyo tutapigania yeyote kati yetu atakayekuwa amepewa ridhaa ya kuwakilisha chama chetu na kwa yule atakayekosa kuteuliwa hatahama kwa sababu ya kutoteuliwa”alisema Kidera.
Kidera, alisema wote wataheshimu
maamuzi ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kwa lengo la kumng’oa nduli CCM
na vibaraka wake.
Kwa upande wake Stephen Kitomary (Chadema),
alisema amepata msukumo wa kugombea Ubunge katika jimbo hilo, kutokana na ukwamishwaji wa shughuli za
maendeleo na mbunge aliyoko sasa.
“Mbunge aliyekuwepo kwa sasa anaishi
eneo la wazi ambalo lilikuwa limetengwa kwa ajili ya kujenga soko, hivyo
kusababisha kutokuwepo kwa soko”alisema
Adolfu Mkono, ambaye ni mwanafunzi wa
Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM), ametambaye anawania udiwani Kata ya Tabata alidai
kuwa anagombea nafasi hiyo kwa ajili ya kupinia haki za wanyonge ambao
wametengwa na viongozi walioko madarakani.
Wakati wanachama hao wakitangaza nia za kutatua kero
za wananchi, mkazi wa Kitongoji cha Kibaoni, Kisarawe Pwani, Raheli Samweli, amekishukuru Chadema kwa
msaada wake wa kumjengea nyumba.
Akizungumza na wandishi wa habari, Raheli Samweli, mama wa familia ya watoto watatu, ambaye kwa sasa ni mjamzito, alisema mahali anapoishi ni hatarishi, hata
hivyo ameomba msaada kwa wadau wengine watakaoguswa wamsaidie.
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana
Bavicha (Bavicha), Kisarawe Baraka
Musa (Chadema), alisema kuwa atahakikisha wanamsaidia mama huyo, ili apate sehemu nzuri kwa ajli ya malazi.
“Tumejipanga Chadema tutahakikisha wananchi wote wanaoishi mazingira mabovu
tunawasaidia”alisema Baraka.
Musa, alisema kutokana na wananchi wa
Kisarawe kuishi mazingira hatarishi ameamua kutia nia ya kugombea
Udiwani Kata hiyo, ambayo kwa
sasa inaongozwa na Adamu Nimba,
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri
Wilaya ya Kisarawe.
Kwa atakayeguswa wasiliana na
0658 15 24 O9.
No comments:
Post a Comment