KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Sunday 5 April 2015

SERIKALI YA AWAMU YA NNE YAJIVUNIA MAFANIKIO ILIYOPATA

Rais Kikwete, akiwa anazungumza na Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani John Kerry

SERIKALI ya awamu ya nne inajivunia mafanikio iliyoyapata tangu kuingia madarakani mwaka 2005 na kuweka msingi imara wa nchi katika kutekeleza mkakati wa maendeleo wa mwaka  2025  unaolenga kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye  uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Rais Jakaya Kikwete alitoa kauli hiyo juzi jijini Washington DC wakati akitoa mhadhara katika Kituo cha Kimataifa cha Woodrow Wilson.

"Naamini mrithi wangu atayaendeleza na kujifunza kutokana na mafanikio haya na kuendeleza kutoka pale tutakapoachia," alisema.

Rais Kikwete, alisema anatarajia Tanzania itakuwa na sera na sheria ya kusimamia gesi na mapato yake kwa vile inatarajiwa kuanza kupatikana ifikapo mwaka 2020.

Katika mhadhara huo uliohudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo mabalozi, wasomi na viongozi wa taasisi hiyo, Rais  Kikwete alielezea mafanikio na changamoto katika uongozi wake wa miaka 10 katika elimu, siasa, uchumi na maendeleo ya jamii.

"Najivunia kuweza kuendelea kuliweka Taifa katika hali ya umoja pamoja na changamoto zote, tumepambana na vitisho pale vilipojitokeza na pia tumetoa mchango mkubwa katika harakati za kisiasa zilizopelekea vyama viwili kutiliana saini maridhiano na kupata muafaka mwaka 2010," alisema.

Rais Kikwete alisema makubaliano hayo yalipelekea Zanzibar kufanya uchaguzi kwa amani na kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa baina ya vyama vya CCM na CUF. 


"Natumaini tutafanya uchaguzi  huru, haki na aman,i ili niweze kumkabidhi urais mrithi wangu katika hali ya utulivu"  alisema Rais.

No comments:

Post a Comment