ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT), Dayosisi Kaskazini, Fredrick Shoo, amewaonya baadhi ya
viongozi wa kiroho na Jamii, kuacha tabia ya kupenda kupokea fedha za aibu ambazo
zinawafanya washindwe kusimamia haki za watu wa mungu.
Kauli hiyo aliitoa wakati wa ibada kuwaingiza
kazini viongozi wapya watatu na kuwaaga wengine wawili, ibada ambayo ilifanyika
katika Usharika wa Azania Front jijini Dar es Salaam jana.
Alizitaja fedha hizo kuwa ni zile zilizopatikana
kwa njia ya rushwa, wizi, dawa za kulevya au hata kama ni kwa njia ya sadaka zinazotolewa
kwa watumishi wa mungu hizo hazikubaliki kwani matokeo yake ni viongozi hao
kupotosha ukweli wa injili.
“Viongozi uwakikosa uaminifu wawe wa kanisa wawe
wa kijamii watakosa nguvu ya kukemea rushwa, wizi na mali ya kanisa watakosa
nguvu ujasiri wa kukemea wizi wa mali ya umma,”alisema.
Askofu Shoo, alisema vitendo vya matumizi ya
fedha ya aibu hayakubaliki kwa yeyote mwenafasi ya kuongoza watu wangu.
Alisema kiongozi bora anapaswa kuwa kielelezo
cha kusimamia haki za wale anaowaongoza na si kujifanya kama vile bwana kwa
kuwalazimisha watu wamfuate.
Viongozi walioingia kazini
Viongozi walioapishwa jana walikuwa ni Askofu
Msaidizi wa Diyosisi ya Mashariki na Pwani, Chadiel Lwiza, Katibu Mkuu Geofrey
Mkini na Naibu Katibu Mkuu Boniphace Kombo.
Dk. Alex Malasusa alipokuwa akiwaapisha viongozi
hao aliwaasa waende wakatoe huduma hiyo ya kiroho kwa kuzingatia kitabu cha
Biblia ambacho ndio muongozo wao.
Walioagwa walikuwa ni Askofu Msaidizi wa
Dioyosisi ya Mashariki na Pwani, George Fupe, ambaye alizawadiwa gari aina ya
Toyota Double Cabeenna na Katibu Mkuu Balozi Richard Mariki, naye pia
alizawadiwa gari aina ya R4.
Akizungumza baada ya kuagwa Askofu Fupe,
aliwaasa viongozi wenzake waliyowapisha kwamba waende wakatafanye kazi hiyo ya
kuwahudumia wa amini kwa kuzingatia ushirikiano.
“Mwanzo nilikuwa nakutuma sasa umekuwa kiongozi
wangu ututume tu na utakapoona tumekosea utusamehe,”alisema Fupe.
No comments:
Post a Comment