KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Wednesday 6 May 2015

MATEBWE:CCM IKATAE WATOA RUSHWA KUPATA UBUNGE

Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philp Mangula
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wilayani Rufiji, Pwani, Shaban Matebwe, amesema wako watu wanaokichafua chama hicho kwa kushiriki waziwazi katika utoaji rushwa ili wapate kuchaguliwa kwenye nafasi za uongozi.
Alisema hivyo kwa vile kuna watu wanaokwenda wilayani hapo kuinadi rushwa waziwazi kwa ajili ya kutaka kuteuliwa na chama ili waje wagombee nafasi ya ubunge na udiwani wakati wa Uchguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salam leo, Matebwe, alisema kuna ulazima wa watu hao wakatambua kuwa msingi wa chama hicho ni kuwatetea wanyonge na masikini hivyo hakitakubali kutoa nafasi kwa wala rushwa.
Alisema hivyo kwa kuwa sheria ya uchaguzi ya mwaka 2010 inakataza wagombea wanafasi ya uongozi katika chama chochote kutoa rushwa, kwa maana hiyo mgombeya yeyote atakaye bainika ametoa rushwa, anaweza kukatiwa rufaa ya kutokuwa mgombea.
“Mgombea wa chama chochote akitoa rushwa ili achaguliwe katika nafasi ya uongozi ikibainika kweli ametoa rushwa inawezekana kabisa akatiwa rufaa ya kutokuwa mgombea,”alisema Matebwe.
Matebwe, alisema kutokana na sheria hiyo, wanachama wa CCM wanapaswa kujihadhari na wagombea wa aina hiyo kwani wanaweza kuja kukipotezea nafasi chama pindi watakapo katiwa rufaa na wapinzani.
Alisema ili kuepuka hayo yasije kukikumba chama, ni vema uongozi wa juu ukatoa onyo ambalo litawafanya watu hao wasiendelee kukichafua na kukidhalilisha chama hicho.
Aidha, alisema kama watu hao wataendelea kukichafua chama kwa mtindo huo basi UVCCM wilayani Rufiji itawaweka hadharani watu hao ambao wanalinyemele jimbo hilo.


Jimbo hilo la Rufiji kwa sasa liko chini ya Seif Rashid ambaye ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii.

No comments:

Post a Comment