MAKALA
HALI ya sintofahamu kuhusu kupewa eneo la kufanyia biashara kwa
wafanyabiashara ndogo ndogo (Wamachinga), kuna madai kuwa ugawaji wa eneo hilo la Jangwani, hauzingatii utaratibu wa kujali
haki za walemavu.
Hivi karibuni wafanyabiashara wa maduka makubwa walikwenda
kumlalamikia Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, kwamba wamachinga walikuwa
wakivuruga biashara zao, kwa kupanga bidhaa zao nje ya maduka yao.
Baada ya malalamiko hayo, Mkrugenzi huyo aliitisha kikao kwa ajili ya
kutafuta muafaka wa mvutano huo, hata huvyo mwisho wa siku ikatokea wamachinga
hao kutakiwa kuhamia Jangwani.
Kwa ujumla baada ya wamachinga hao ambao wamechanganyika na watu
wenye ulemavu, kupata taarifa hizo, wale wenye viungo kamili walikwenda kuvamia
maeneo ambayo wanaona yanafaa.
Kuvamia huko kulitokana na kutokuwepo utaratibu wowote uliyokuwa
umepangwa na viongozi wa manispaa hiyo.
Utaratibu huo mbovu ulisababisha watu wenye ulemavu washindwe kupata
maeneo hayo ambayo pia yameingiliwa na matapeli.
Matapeli hao baada ya kusikia kuwa wafanyabiashara wameruhusiwa
kufungua bishara zao, walifika mapema na kushika maeneo ambayo hivi sasa
wanayauza kati ya sh. 180,000 hadi sh. 300,000.
Hali hiyo imewafanya watu wenye ulemavu kuendelea kuteseka kutokana
na kushindwa kupata fedha, hizo ambazo wakizitowa watakuwa wameua msingi wa
biashara zao.
Matapeli hao bila aibu wamejivika uhalisia wa kuwa wamiliki wa maeneo,wakidai
ni ya kwao hivyo kila anayetaka lazima awaone wao bila hivyo hakuna atakayepa.
Labda, ni kichangia klatika hili naweza kusema kwanza uongozi wa
manispaa ya Ilala imekosea kwani haikuweka utaratibu mzuri akatika ugawaji wa
maeneo hayo.
Baadhi ya wandishi siku wamachinga hao wanakwenda katika eneo hilo
bahati mbaya hakukuwa na kiongozi wa aina yeyote ambaye angeweza kutoa
malekezo.
Hali hiyo ndio imesababisha vurugu zote hizo kwa mtu mmoja kumiliki maeneo
makubwa na kuanza kuwauzia wengine kinyume cha sheria.
Kinachoshangaza hadi naadika makala haya hakuna kiongozi hata mmoja aliyefika kujionea
maendeleo ya wafanyabiashara hao.
Pamoja na nia njema ya serikali ya kuwasidia wafanyabiashara, ili
wafanye biashara zao kwa amani lakini bado kuna maswali mengi kuhusu eneo hilo.
Maswali hayo yanatokana na ukweli kwamba eneo hilo bado halina huduma
za kijamii kama vile vyoo na mabomba ya maji jambo linalowashangaza wananchi.
Inaonekana uongozi wa wilaya hiyo umekurupuka kwani haikuwa na mpango
wa kuwapeleka pale isitoshe haieleweki eneo hilo litakuwa la kudumu kwa
wafanyabiashara hao au la.
Maswali hayo yanatokana na ukweli kwamba eneo hilo waliwahi kupewa
madereva wa Fuso kama eneo lao la kuegeshea magari baada yakutotakiwa kuonekana
katikati ya jiji.
Madereva hao walipwa eneo hilo kwa sherehe kubwa na aliyewahi kuwa
Mkuu wa Mkoa huo, Yusufu Makamba, tena wakati huo pakiwa pamejengwa miundombinu
muhimu.
Makamba, aliwajengea vyoo, mabomba ya maji na kituo cha Polisi, hata
hivyo katika mazingira tata madereva hao walikuja ondolewa na Mkurugezi wa jiji,
bakari Kingobi kwa madai kuwa madai kuwa walipelekwa kimakosa na kwamba alikuwa
hawatambui kwa vile hawakuwa na nyaraka zinazothibitisha uwepo wao.
Nimekumbushia hilo, nikiwa na maana kwamba utaratibu uliotumika
unatiashaka kwamba huenda kupelekwa pale ikawa ni mtego ili baadae waje
kuwaondoa tena kwa visingizio vyovyote wakati huo.
Ili kuepuka mgogoro mwingine ni vema uongozi ukajitokeza
kuwahakikishia wafanyabiashara hao kwamba haita waondoa kama walivyowaondoa
madereva wa maroli.
Uongozi huo uwaeleze kuwa eneo lile hivi sasa linatumika kinyume na
awali kwamba lilikuwa eneo la bondeni na hatarishi kwa sababu za kuitwa hivyo
bado zipo na kubwa zaidi ni mvua.
Ushauri wangu kwa machinga ni kwamba wasiwekeze nguvu zao zote kwa
kuamini kwamba huenda wakaishi hapo milele wanaweza kuja kujuta kwani serikali
hii ni kigeugeu, ambayo haijali matatizo ya wananchi wake.
No comments:
Post a Comment