MAKALA
WAZAZI wenye watoto katika kituoni cha kulelea watoto
wenyemahitaji maalum Buhangija mkoani Shinyanga wamewatelekeza watoto hao kwa
zaidi ya miaka sabab sasa.
Watoto hao ni wale wenye ulemavu wa ngozi (Ualbino), ambao
wamewapeleka kituoni hapo kwasababu huko vijijini watoto hao wanawindwa na
wauwaji kutokana na imani za kishirikina.
Kutokana matukio ya kuwindwa watoto hao na wao kuogopa kufanyiwa
vitendo vya kikatili hivi sasa kituo hicho kimekuwa kikipokea watoto watatu
hadi watano kila siku kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa ya kanda ya Ziwa.
Kutokana na ongezeko hilo, kituo hicho kinakabiliwa na matatizo
mengi ikiwemo kukosefu wa huduma za kijamii huku baadhi ya wazazi wa toto hao
hawajulikani waliko kwani hata anuani walozoacha awali hazipatikani na hata
maeneo waliyokuwa wakiishi wamehama bila ya taarifa.
Kituo hicho awali kilikuwa kikipokea fedha kutoka serikalini
ambapo bajeti inayotengwa ni kwa ajili ya watoto 50, hata hivyo fedha hizo kwa
sasa hazitoshi kutokana na wingi wa watoto kituoni hapo.
Hivi karibuni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknoloji, January
Makamba, akiwa Shinyanga kutafuta
wadhamini, wananchi waeneo hilo walimuomba ende kituoni hap kwa ajili ya
kujionea maisha ya watoto hao.
Makamba alifanya mazungumzo na wadau kadhaa wa harakati za
kupinga mauaji ya albino, ndipo akatajiwa kituo hicho.
Baada ya kutajiwa kituo hicho alikubali kutembelea kituo hicho baada
ya shughuli ya kupata udhamini kukamilika, kwamba angetumia walau hata nusu saa
katika kituo hicho cha Buhangija.
Kutokana na hali ya kukatisha tamaa aliyoikuta kituoni hapo
Makamba na msafara wake wakiwemo wandishi wa habari walikaa saa tatu.
Yote hayo yalitokana nakuguswa na mazingira na changamoto za
kituo kile, zaidi na upendo wa watoto wale kwa kuwa saa zote walipenda kubebwa
na kushikwa na kukumbatiwa.
Kwa asiyejua hali ya maisha ya watoto hao katika kituo hicho,
basi ni vema mkatambua kuwa kinahitaji msaada mkubwa.
Katika kituo kile kuna shida ya kila kitu ikiwemo mabweni,
vitanda, magodoro, shuka, vyandarua, mashuka, madawa - kila kitu, lakini shida
kubwa zaidi ni vyakula.
Kwa siku kituo hicho kinatumia kilo 70 za unga/mchele, kilo 70
za maharage, bado mafuta, sukari na maji ambako Mkaa unaotumika kwa siku ni
gunia moja na nusu. Makamba katika kutembelea kituo hicho kuwa watoto hao wana ndoto
kubwa za maisha yao ya baadae, lakini pia wanajua kwamba maisha yao yako
hatarini na wale wadogo zaidi wanapata shaida kuelewa ni kwa nini.
Baada ya kuzungumza na walimu kuhusu kuwa na utaratibu endelefu
wa kupata rasilimali za kuendesha kituo hicho, na kwamba kuna mawazo kadhaa ya
kufanyiwa kazi.
Aidha, kutokana na matatizo hayo makubwa yaliyoko kituoni hapo
bado misaada inahitajika hivyo basi kama yupo atakayeguswa wasiliane na Mwalimu
Peter Ajari kwa namba ya simu 0757 611 930.
Nikiwa mmoja wa wandishi waliofika kitoni hapo niseme tu kwamba
hali katika kituo hicho ambacho kina watoto zaidi ya 300 hali ni mbaya hivyo ni
wakati kwa jamii kuwakumbuka watoto hao.
Mtoto mdogo kuliko wote katika kituo hicho ana miezi 18 na
mkubwa zaidi ana miaka 24, ukiongea nao, wana ndoto kubwa za maisha yao.
Hata hivyo kuna haja ya kuwapongeza baadhi ya wafadhili na
taasisi ambazo zimekuwa zikisaidia kituo hicho kwa mfano kuna taasisi zimeajiri
walimu na walezi wa ziada.
Mwisho ni ungane na kauli ya Makamba kwamba hata kama huna cha
kutoa basi ukifika Shinyanga, usiache kutembelea Buhangija kwasababu watoto
hawa wanahitaji pia upendo, kwani wengi wao wazazi wao walivyowaacha hawajarudi
tena.
Makamba, katika ziara yake hiyo, alitoa msaada wa unga wa sembe
kilo 500, maharage kilo 500, mchele kilo 500, mafuta ya kula, sabuni na vitu
vingine.
Pamoja na yote hayo, nawasihi wazazi waliowatekelekeza watoto
kubadili msimamo huo, na baadala yake wajitokeze katika kutoa ushirikiano wa
kimalezi kitendo ambacho kitawaletea faraja watoto hao.
No comments:
Post a Comment