MBUNGE wa Jimbo la Singida Mjini kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) anayemaliza muda wake, Mohammed Dewji (Mo) ametangaza kustaafu rasmi siasa na kutogombea tena ubunge
baada ya kuliongoza jimbo hilo
kwa miaka 10.
Dewji alitangaza uamuzi huo jana, katika Viwanja vya Peoples Club mjini hapa
huku akishuhudiwa na umati mkubwa wa watu
waliofurika kutoka kila pembe ya
Singida mjini.
Alisema amechukua uamuzi
huo baada ya kulitumikia jimbo hilo kwa muongo mmoja hivyo ameamua kutoa fursa kwa makada wengine
wa chama hicho kuendeleza mazuri aliyoyafanya katika kipindi cha ubunge wake.
Alibainisha kuwa kutokana na kubanwa na majukumu mengine
ameamua kwa ridhaa yake mwenyewe pasipo
kushinikizwa na mtu yeyote kuachia jimbo.
“Nimeamua kwa ridhaa
yangu kutangaza kutogombea tena ubunge katika jimbo hili ili kutoa nafasi kwa
makada wengine wa CCM Singida Mjini kuwania nafasi hiyo,” alisema.
Alisema alipoanza safari
yake ya siasa, lengo kuu lilikuwa kuleta
matumaini kwa watu wa Singida mjini kwa sababu
palipo na matumaini kila kitu kinawezekana hivyo uamuzi wa kutogombea unabaki palepale .
Mafanikio
Akizungumzia mafanikio, alisema katika ubunge wake alijenga
shule 15 za sekondari za kata kutoka
mbili alizozozikuta mwaka 2005. Pia alisaidia watoto 15,000 ambao wazazi wao
hawana uwezo katika masomo yao
na kujenga Zahanati za Mungumaji na
Manga ambazo zimekamilika na katika Kijiji cha Ititi bado ujenzi
unaendelea.
Alisema alijenga vyumba
vya madarasa pamoja na kusambaza madawati katika shule zote za msingi katika
jimbo lake. Pia alitoa vyandarua zaidi ya 6,000 kwa ajili ya kinamama na watoto
jambo ambalo limeonyesha mafanikio kwa asilimia 50, na kupeleka madaktari bingwa ambao waliweza kufanya upasuaji kwa
watu 1,000 waliougua mtoto wa jicho.
No comments:
Post a Comment