Mwenyekiti na Muasisi wa Chama cha Kijamaa na Uzalendo Tanzania (CKUT), Ramadhani Semtawa, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama hicho, Noel Antapa |
MWENYEKIT
wa Chama cha Kijamaa na Uzalendo Tanzania (CKUT), Ramadhani Semtawa,
amesema chama hicho kitarajia kushiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25
mwaka huu.
Chama
hicho kilipta usjili wa muda tangu Aprili 13 mwaka na kilpaswa kupata usajili
wa kudumu ndani ya miezi sita, baada ya kupata wanachama katika mikoa kumi
nchini.
Semtawa, aliyasema hayo wakati alipozungumza
na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu kama chama hicho
kitashiriki uchaguzi huo au la.
Alisema
hivyo kwa vile hadi sasa chama hicho kimemaliza kazi ya kupata wanachama katika
mikoa kumi nchini, kati ya hiyo miwili ikiwa ni kutoka Zanzibara, tayari
wamekwisha kabidhi makablasha ya wanachama hao kwa Msajili wa Vyama tangu Julai
1 mwaka huu.
Aliitaja
majina ya mikoa walikokwenda kupata wadhamii hao kuwa ni pamoja na Dar es
Salaam, Pwani, Tana, Tabora, Lindi, Mtwara, Dodoma, Morogoro kwa upande wa Bara
na Kusini Pemba na Mjini Magharibi Tanzania Zanzibar.
Semtawa,
alisema baada ya hatua hiyo wanamsubiri utaratibu wa Msjili wa kuhahakiki,
baada ya kuwaona wanachama hao, atato cheti cha usajili wa kudumu, ambacho
kitawafanya washiriki uchaguzi huo.
“Kimsingi
chama hicho kinaimani kubwa na Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa chini ya
Jaji Francis Mutungi na wasaidizi wake
Sisty Nyahoza, hivyo tunaimani uhakiki utakwenda vizuri tu.
“Baada ya hapo tutakuwa tumekamilika kichama,
tutaweza kusimamisha wagombea katika majimbo na Kata lakini kwa sasa tuna uhuru wa kupeperusha bendera,
kufungua matawi na kufanya mikutano ya hadhara,”alisema Semtawa.
Semtawa,
lisema shabaha yao kubwa katika uchaguzi huo ni kusimamisha wagombea katika
udiwani na umbunge kwa lengo la kuzishika Halmashauri.
“Sisi
tuko tayari bali tunamsubiri Msjili wa Vyama atuite wakati wowote kuanzia hata
kesho kwa ajili ya kuhakiki majina hayo kwani akifanikiwa katika kipindi hiki
cha Julai mwaka huu, tutaweza kwenda sambamba na ratiba ya uchaguzi
huo,”alisema Semtawa.
Alisema,
Ratiba ya uchaguzi huo inaonesha kuwa Agosti 22 mwaka huu ndio siku ya kuanza
kampeni.
No comments:
Post a Comment