KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Friday 31 July 2015

WAMACHINGA JANGWANI WAGOMA KUONDOKA

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi
WAFANYABIASHARA, wadogo wadogo (Wamachinga), wanaotakiwa kuondoka katika eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam, wamekimbilia Mahakamani kuweka zuio la kuondolewa katika eneo hilo.
Hatua hiyo inafuatia agizo la Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akishirikiana na Mkurugenzi wa wilaya hiyo Issaya Mngurumi, la kuwataka kuondoka katika eneo hilo kwa madai kuwa ni wavamizi.
Akizungumza na wandishi wa habari katika eneo hilo, Mtunza Fedha, wa Wafanyabiashara hao, Paschal Kalo, alisema kuwa wanapinga agizo hilo kwa vile uongozi wa Manspaa hiyo ndio ulihusika katika kuwapeleka pale.
“Tunashangaa kusikia kuwa mkuu wa wilaya na mkurugenzi kutuita sisi wavamizi jambo ambalo halina ukweli wowote, hatuwezi kuondoka kirahisi bila kuhakikishiwa jinsi tutakavyorejewagharama zetu na kuelekezwa pa kwenda,”alisema Kalo.
Kalo, alisema wanapinga kuondoka kwa vile wamekwenda katika eneo hilo kutokana na makubaliano kati yao na mkuu wa wilaya na mkurugenzi.
Jangwani, akibainisha kuwa hakuna waliotoka sehemu nyingine kama walivyodai.
Kuhusu madai kuwa walikubaliana wasijenge mabanda, alisema katika hilo alipinga, ukweli ni kwamba walikubaliana kujengwa mabanda na ndio maana uongozi wa manispaa hiyo ukaahidi kuwafikishia huduma ya umeme.
“Kama hatukuruhusiwa kujenga mabanda, huo umeme waliotuahidi wangekwenda uweka chini au kwenye miamvuli hebu viongozi wetu wawe wakweli wasitafute kuwanyanyasa raia huku wakijua walichokifanya,”alisema Kalo.
Mgogoro kati ya wamachinga na uongozi wa wilaya hiyo umeibuka baada ya Baraza la Hifadhi ya Mazingira (NEMC), kuitaka Halmashauri hiyo kusitisha ugawaji wa eneo hilo, kwa vile si salaama kwa maisha ya binadamu.

No comments:

Post a Comment