Dk. Mahanga, akionesha kura feki, wakati alipozungumza na wandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. |
KADA wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Dk. Milton Makongoro Mahanga, ametangaza kujivua uanchama wa
chama hicho, anakusudia kujiunga na Chama cha Demeokrasia na Maendeleo
(Chadema).
Dk. Mahanga, alisema
amefikia uwamuzi huo baada ya baadhi ya vigogo kuanzisha operesheni ya
kumuondoa katika ubunge Jimbo la Segerea.
Akizungumza na
wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Dk. Mahanga, alisema katika ushindani
wowote kuna kushinda na kushiwandwa, kama angeshindwa kwa halali wala
asingekuwa na kinyongo chochote.
Alisema amefikia
hatua hiyo kutokana na mfumo mbovu wa CCM unaowapa viongozi wachache uhalali na
kiburi cha kufinyanga demokrasia na kuendeleza dhuluma.
Dk. Mahanga, alisema
mfumo pamoja na hila umekuwa ukiwanyima haki baadhi ya wagombea bora hivyo kukiangamiza taratibu chama hicho.
“Niweke wazi kwamba
sina ugomvi hata kidogo na wanachama walio wengi wa CCM katika jimbo la Segerea
amabao kwa miaka 15 wamenipa ushirikiano mzuri sana katika kuleta maendeleo
katika jimbo hili la Segerea ikiwemo barabara,”alisema.
Aidha, alisema katika kura za maoni za kuwapata wagombea wa
udiwani na ubunge katika jimbo hilo, kulikuwa na upendeleo wa wazi hususan kwa Bonna Kalua.
Dk. Mahanga, alisema mazingira na ushahidi
mbalimbali ulonesha ni jinsi gani Bonna alivyobebwa na wizi wa kura uliofanywa
na mgombea huyo na washirika wake hadi kuugeza uchaguzi huo kuwa kituko mbele
ya wanachama wengi wa CCM.
Alisema licha ya
malalamiko mengi aliyotoa kwa mdomo, simu na barua, uongozi wa CCM wilaya, Mkoa
na Taifa haukuchukua hatua zozote za maana na yaonekana wazi uongozi huo
ulikuwa sehemu ya mpango mzima wa kuhakikisha anashindwa katika uchaguzi huo. x “Rejea barua zangu
kwa Katibu wa wilaya na Katibu Mkuu, kama vile barua Kumb. SEG/CCM/02/14 ya
tarehe 28/72014; SEGCCM/03/14 ya tarehe 04/08/2014; SEGCCM/04/14 ya tarehe
19/8/2014; SEGCCM/05/14 ya tarehe 19/8/2014 na SEGCCM/01/15 ya
21/01/2015,”alisema Dk. Mahanga.
Dk. Mahanga, alisema
kule Dododma kuna familia ya kigogo mkubwa wa CCM Taifa ambaye hakuweza kumtaja
jina, iliyokuwa ikiishi jirani na nyumbani kwake iliamua hata kuisakama familia
yake.
Alisema familia hiyo
ya kigogo ilifikia kuwaeleza wanaye kwamba baada ya kuondoka Waziri Mkuu wa
zamani Eduard Lowssa sasa itakuwa ni zamu ya baba yao kuondoka Segerea kwa
gharama yeyote.
Dk. Mahanga, alisema
baada ya kauli hizo ndipo fedha nyingi ziliingizwa jimboni kwake na kufikia mikononi mwa Bonnah amabye
alianza kuzigawa kwa wingi na jeuri kupindukia.
Alisema
baada kuingizwa fedha hizo, ghafla walikuja wagombea wengine wapya ambao
wengine walijidai kwamba wametumwa kwa kazi maalum ya kumzuia Dk. Mahanga
kushinda ubungea kwa kugawa zile kura.
Dk. Mahanga alisema kuwa kura
amabzao zilionekana wazi zingekuwa za kwake ili kumpa Bonnah nafasi kubwa ya
jushinda kura hizo za maoni.
Aliongeza kwa kusema
kuwa licha njama zote alizozitaja hapo juu kuumbeba Bonna, bado njama
zilifanyika za kumpa kura za wizi, na makaratasi mengi ya kura yaliyotolewa
kwenye maeneo ambapo yalikuwa tayari yamewekewa alama ya vema kwenye jina la
Bonnah.
“Mfano ni kitabu cha
karatasi za kura Na. 4401-4500 na 27801-27900 ambavyo ni sawa na kura 200
zilizokamatwa maeneo ya Kata ya Kinyerezi. “Yaonekana maelfu ya
karatasi kama hizi zilitumika maeneo mengi ya jimbo kumpa ushindi wa bamdia
Bonnah,”alisema Dk. Mahanga.
Alisema fedha katika
kura hizo ziligawanywa katika jimbo hilo hadi siku ya kupiga kura, baadhi ya
maeneo wanachama walipewa sh. 10,000 kila mmoja huku wengine wakipewa kadi mpya
hususan vijana wakipewa kadi mpya zenye majina feki.
MJUWE DK. MAHANGA
Dk. Milton Makongoro Mahanga
amezaliwa katika kijiji cha Mugeta wilaya ya Mara Kusini (sasa Bunda) Aprili 3, 1955. Akina mama wawili wa kabila la Waikizu waliomsaidia mama yake kujifungua, waliwaomba wazazi wake wakubali kunipa jina la Makongoro ambaye alikuwa Chifu wa Waikizu ingawa asili yake ilikuwa ni wilaya ya Mara Kaskazini (sasa Rorya).
Wazazi wake walikubali na mpaka sasa anatumia jina hilo la Makongoro.
Wazazi wake walikubali na mpaka sasa anatumia jina hilo la Makongoro.
Baadaye walihamia wilaya ya sasa ya Serengeti ambako alisoma katika Shule za Msingi za Kyambai (sasa Matare) na Mugumu katika wilaya hiyo ya Serengeti na Bukama Ikizu katika wilaya ya Bunda kati ya mwaka 1965 na 1971.
Mwaka 1972 hadi 1975 alisoma kidato cha Kwanza hadi cha Nnne katika Shule ya Sekondari Mara na baadaye kumaliza masomo ya Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Tambaza jijini Dar es Salaam.
Kuanzia mwaka 1978 hadi 1980 alichukua masomo ya Shahada ya Kodi na Uhasibu katika Chuo cha Fedha (IFM), jijini Dar es Salaam. Kupitia Bodi ya Ununuzi na Ugavi ya NBMM (sasa PSPTB) nilikuwa Mtanzania wa kwanza kupata Stashahada ya Juu ya Ununuzi na Ugavi CSP (sasa CPSP) inayotolewa na NBMM mwezi Mei 1980.
Aidha kwa mara nyingine alikuwa Mtanzania wa Kwanza kuwa na CSP na CPA kwa pamoja pale alipofanikiwa kupata Stashahada ya CPA inayotolewa na Bodi ya Uhasibu (NBAA) mwezi Mei 1983. Baadaye, akiwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) niliamua kusoma na kutunukiwa cheti cha uzamili kwenye masuala ya fedha (MSc Finance) mwaka 1997 kupitia Chuo Kikuu cha Strathclyde cha Glasgow nchini Uingereza.
Kupitia utafiti wa kina nilioufanya nchini Tanzania na nchi nyingine kama Uingereza, Kenya na Uganda kuhusu mahusiano kati ya umasikini na makazi duni mijini, nilifanikiwa kutunukiwa Shahada ya uzamivu (PhD) kupitia Chuo cha Washington International University cha nchini Marekani Julai mwaka 2000. Kwa umahiri wake, utafiti wangu huo uliweza kuchapishwa mwaka 2002 na wachapishaji wa Dar es Salaam University Press (DUP) kama kitabu: “Urban Housing and Poverty Alleviation in Tanzania” kwa namba ISBN 9976-60-343-6.
No comments:
Post a Comment