KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Wednesday 5 August 2015

WATU WENYE ULEMAVU WATOA YA MOYONI

KUNDI la watu wenye ulemavu jijini Dar es Salaam, limesema kuwa ushiriki wao katika kugombea nafasi za uongozi ndani ya vyama vya siasa unakabiliwa na vikwazo vingi ikiwemo kutengwa kutokana na hali zao.
Hayo yalielezwa jijini, Kiongozi wa kundi hilo, Athuman Sembe, wakati walipokusanyika kwa ajili yakupatiwa elimu ya kuhusu uchaguzi mkuu na Taasisi ya kutoa elimu juu ya uchaguzi ya Amosi Joseph (TEAJ).
Alitaja vikwazo wanavyokumbana navyo katika kipindi hiki ni mabaya ya madaraka kwani baadhi ya viongozi wa baadhi ya vyama wamekuwa wakitoa nafasi kwa wagombea kwa kujali zaidi uhusiano wa kidugu.
Sembe, alisema licha yakupeana nafasi hizo kidugu bado pia kumekuwa na matumizi makubwa ya rushwa kitendo ambacho kimekuwa kikiwanyima haki katika kushiriki chaguzi mbalimbali.
"Ukiangalia katika vyama vyote utagundua kwamba watangaza nia wa kundi hilo ni wachache mon hali inayodhihirisha wazi kuwa kundi hilo limetengwa,"alisema Sembe.
Joyce Charles, alisema kuwa kundi la wanawake, vijana ni moja ya sehemu ambayo imekuwa ikisahaulika kwa kasi kibwa ingawa kuna taarifa kwa upande wa Zanzibar vyama vimeweza kufanya vizuri.
Alisema kwa mfano hata mkienda kwenye vyama hivyo vya siasa na kukiuliza kila kimoja kina wagombea wangapi wa watu wenye ulemavu utakuta majibu yatakayotolewa ni ya kubuni, kwani havina utaratibu wa kuweka kumbukumbu za kundi hilo.
Naye Mkurugenzi wa (TEAJ), Amos Joseph, alisema kuwa amebaini kwamba bado vyama vyote vya siasa nchini havijatoa nafasi sawa katika ushiriki wa mchakato wa kuwapata wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi.
Alisema kundi hilo lina haki ya kushirikishwa katika kila hatua inayohusu masuala ya uongozi ikiwa ni katika ngazi ya maamuzi.

Joseph, alisema baada ya kupokea matatizo hayo, taasisi yake itayafanyia kazi kwa karibu ikiwa ni pamoja na kukutana na baadhi ya viongozi wa vyama hivyo. 

No comments:

Post a Comment