KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Wednesday 5 August 2015

BOMBA LA GESI LA KAMILIKA ASILIMIA 100


WAZIRI wa Nishati na Madini, George Simbachawene amesema ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Kituo cha Kinyerezi (1) umekamilika kwa asilimia 100.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Simbachawene alisema mtambo wa umeme wa Kinyerezi namba moja  utaanza majaribio kuanzia mwisho wa mwezi Agosti hadi Septemba mosi mwaka huu.
Alisema baada ya kukamilika kwa kazi hiyo shughuli itakayofata ni kuunga bomba wote wa megawati 150 wa Kinyerezi kwenye gridi ya taifa na kuanza rasmi uzalishaji wa umeme sambamba.
“Kukamilika kwa mradi huu wa bomba la gesi kutatuhakikishia upatikanaji wa umeme kwa uhakika ambao utatushelezea mahitaji yetu, hususani katika maswala ya viwanda,”alisema Simbachawene
Simbachawene alisema kazi hizo za majaribio ya bomba la gesi na mtambo wa kinyerezi, kazi nyingine zinazoendelea itakuwa nikukamilisha ujenzi wa njia ya umeme ya km 2.8 ya msongo wa kilovoti 132 kutokea kinyerezi kwenda kwenye kituo cha Gongo la Mboto.
Alijiridhisha na ametoa maagizo kwa watendaji wote usiku na mchana kuona lengo hilo linatimia kwa hali na mali na pia amewaomba Watanzania wawe wavumilivu kwani wakati kazi hizo zinapokua  zinaendelea baadhi ya Mikoa itaathirika kwa kukosa umeme.  
“Tunaomba wananchi watuvumilie katika kipindi hiki wakati kazi hizo zinaendelea hasa ikizingatiwa kwamba mitambo hii mipya ndio mwanzo mpya wa kuondokana na matatizo ya umeme nchini”alisema.
Tunategemea miradi hii ikikamilika, itazinduliwa rasmi na Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


No comments:

Post a Comment