UMOJA
wa Wakaanga Samaki katika Soko la Feri Dar es Salaam (Uwasaso), wamepatiwa
majiko 48 ya gesi ambayo yatawasaidia kuondokana na utumiaji wa majiko ya kuni
ambayo hutoa moshi mwingi, hatari kwa afya zao.
Kwa
muda mrefu Wakaanga samaki hao wamekuwa wakifanyakazi katika mazingira magumu
kutokana na matumizi ya majiko ya kuni ambayo yamekuwa yakichangia uchafuzi wa
mazingira katika eneo hilo ikiwemo Ikuku.
Akizungumza
namwandishi wakati akiwa katika shuguli zake za uzalishaji jijini leo, Mwenyekiti
wa Uwasaso, Cyril Nyange, alisema majiko hayo yametengenezwa na Kampuni ya Envotech
Tanzania Limited ambayo wameyakubali kutokana na ubora wake ukilinganisha na ya
awali yaliyokuwa yakitumia mkaa.
Alisema,
majiko hayo yanatarajiwa juanza kutumika Machi 15 mwaka huu, baada ya
kukamilika uezekaji wa paa la jengo la jiko hilo la samaki kama ilivyoagizwa, Naibu
Waziri wa Tamisemi Seleman Jafo.
Alisema,
kutokana na ubora wa majiko hayo, wanatarajia kuwa yatasaidia kuboresha
uzalishaji zaidi huku yakiimarisha usafi wa mazingira, hali ya afya zao na kuongeza
wateja ukilinganisha na sasa.
“Waziri
alikuja hapa na kuwaagiza uongozi wa Manispaa ya Ilala kuwa inahakikisha majiko
hayo ikifika tarehe hiyo lazima yaanze kazi huku akiwahakikishi kuwa atakuwepo
katika soko hilo siku hiyo.
“Pamoja
na kuwa karibu Ikulu, tumekuwa tukitumia kuni ambazo moshi wake mbali na
kuathiri afya zetu lakini pia ulikuwa ukiingia Ikulu.
“Yatakapoanza
kazi watu wataupenda kwani tutakuwa tunavaa suti kama vile tuko katika ofisi
kubwa hakutakuwa na moshi labda mvuke kidogo wa mafuta,”alisema Nyange.
Nyange,
alisema hivi sasa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ya Ilala, Issaya Mngurumi, yuko
katika mazungumzo na kampuni za usambazaji wa gesi ili kupata gesi ya kuanzia
katika majiko hayo.
Jiko
hilo lina umuhimu mkubwa kwa vile linahudumia karibu mikoa yote iliyoko nchini,
hivyo kuimarika kwake kutapunguza kero ya foleni wateja wanaofika kwa ajili ya
uzalishaji wa wasamaki wanapotoka baharini.
No comments:
Post a Comment