BALOZI wa Kuwait nchini, Jasem
Alnajem, juzi amezindua kisima chenye urefu wa mita 90 kwa ajili ya matumizi ya
wakazi wa Mtaa wa Golani, Kimara, Kinondoni jijiini Dar es Salaam.
Mtaa huo wenye wakazi zaidi ya
12,000 unakabiliwa na tatizo la maji, barabara pamoja na huduma nyingine za
kijamii tangu ulipoamzishwa miaka nane iliyopita.
Ujenzi wa kisima hicho
umefadhiliwa na kikundi cha wahisani kutoka Kuwait, ambao walifikia hatua hiyo
baada ya kufahamishwa tatizo hilo na Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea
ambaye aliongoza uzinduzi huo.
Katika uzinduzi huo, Balozi
huyo alisema baada ya kukamilisha ujenzi huo nchi yake inatarajia kuchimba
visima vingine katika mtaa huo ambao ameteuliwa kuwa mlezi wake.
“Baada ya kukamilika mradi huu
ni waahidi kuwa huu siyo mwanzo bali tutaendelea kusiriki katika miradi mingine
ya maendeleo hususan baada ya mbunge wenu kutujulisha matatizo yenu,”alisema.
Aidha, Alnajem alisema hivi
karribuni wataanza ujenzi wa kisima kingine huku akiahidi kumalizia ujenzi wa
msikiti ambao umeanza kutokana na michango midogo yaw a umini wa dini ya
Kiislamu wa mtaa huo.
Mbunge wa Ubungo Kubenea,
aliwaasa wakazi wa mtaa huo kuutumia mradi huo wa maji ili uweze kuwasaidia kwa
muda mrefu.
“Nina mawasiliano mazuri na
ubalozi huo kwa hiyo niko tayari kufikisha matatizo ya wapiga kura wangu kwa
balozi huyu, kila nitakapo yapata baada ya kuhakikishiwa naye kuwa milango iko
wazi,”alisema Kubenea.
Bahati Juma, mkazi wa mtaa huo,
alisema upatikanaji huduma hiyo ya maji wa shida kwani wamekuwa wakitembea
mwendo mrefu kufuata huduma hiyo huku maji ya mifereji ambayo siyo salama kwa
afya zao.
“Wakati mwingine tunaletewa
maji ya kununua yale mifereji ndoo sh 300 na ya bomb ash 500 kitendo ambacho
wakati mwingine baadhi yao wanashindwa kununua kutokana na kukabiliwa na
umasikini,”alisema.
Alisema, anaamini kuzinduliwa
kwa mradi huo kutasaidia kupunguza tatizo hilo huku wakisubiri miradi mingine
mikubwa ya serikali.
Hasan Makamba, alisema kwa vile
maji mi moja ya haki za binadamu kwa hiyo wameshukuru kupata kisima hicho kwani
kitasaidia kupunguza bajeti kubwa waliyokuwa wakitumia kwa ajili ya kununua
maji kila siku.
Mwenyekiti wa Mtaa huo, Laurent
Mtoi, alisema mtaa huo uko mpakani mwa wilaya ya Kinondoni na Ilala lakini
kutokana na ubovu wa barabara zinazoelekea Kinondoni kunawafanya wakazi wa mtaa
huo kukimbilia huduma zote za kijamii katika wilaya ya Ilala.
Kwa hiyo ameiomba serikali
kuharakisha ujenzi wa miundombinu yote yenye masilahi na jamii ikiwemo
kukamilisha ujenzi wa shule ambayo hadi sasa vyumba vitano vya madarasa
vinahitajika.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment