KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Friday 6 May 2016

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KUWEKA MAZINGIRA BORA KWA AJILI YA SEKTA BINAFSI

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imeahidi kuweka mazingira bora yatakayo wezesha sekta binafsi kuchangia ukuaji wa uchumi waviwanda katika visiwa hivyo.
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko, Zanzibar, Amina Salumu Ally, aliyasema hayo mjini hapo wakati Jumuiya ya Wakulima, Wafanyabiashara na wenye Viwanda ya Tanzania bara TCCIA na ile ya Zanzibar ZCCIA zilipoingia makubaliano ya kushirikiana kuendeleza sekta za biashara na viwanda kwa karibu.
Makubaliano hayo yalitokana na mikutano iliyofanyika awali kwa kuwakutanisha viongozi wa vyama hivyo, iliyofanyika hivi karibuni.
Alisema serilikali imefikia hatua hiyo kwa vile inatambua umuhimu wa sekta binafsi katika kuchangia maendeleo ya biashara na viwanda nchini.
“Nia ya serikali ya Zanzibar ni kuona Zanzibar ina kuwa ya viwanda na kuifanya inakuwa kituo kikuu cha kibiashara katika nchi zote za jirani.
“Niwapongeze kwa hatua mliyofikia kwani imefungua ukurasampya ambao utasidia kukuza biashara hususan kwa wanawake tena kwa kujianzishiaviwanda vidogovidogo,”alisema Amina.
Aidha, Amina aliwataka watendaji wa serikali kupunguza urasimu wa katika kukaribisha wawekezaji wanaotaka kuwekeza Zanzibar kwani endapo wataendelea kuweka vikwazo visivyo na sababu za kueleweka basi kunaweza kuwakimbiza wawekezaji.
Mkurugenzi Makazi wa Trade Mark East Afrika, alisema kutiliana saini huko, kutasaidi kupunguza vikwazo ambavyovilikuwa vikiwakabili wafanyabiashara.
Alisema, kwani kuna wakati baadhi ya wafanyabiashara wa Zanzibar walikuwa wakikumbwa na changamoto mbalimbali za kufayabiashara zao kutoka sehemu moja hadi nyingine.    

No comments:

Post a Comment