MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA, ISAYA MNGURUMI |
BAADHI ya wafanyabiashara wadogodogo (Wamachinga), wanaofanya
shughuli zao katika eneo la Posta wamelalamikia uwamuzi wa Mkurugenzi wa
Manispaa ya Ilala, Isaya Mngurumi kwa kushindwa kwake kuwapangia eneo la kwenda
kufanyia biashara.
Malalamiko yao yanakuja siku mbili baada ya mkurugenzi huyo
kutoa agizo la kuwataka wa wafanyabiashara hao kuondoka kwa hiyari yao katika
maeneo ambayo siyo rasimi, kuelekea kwenye maeneo yaliyoandaliwa.
Walisema hayo jijini leo,
wafanyabiashara hao, walishangazwa na
uwamuzi wa Mngurumi ambaye wanadai alishindwa kufafanua kwamba wafanyabiashara
hao waelekee wapi kuanzia kesho.
Ramadhan Rajab, alisema wamefikia hatua hiyo baada ya kusikia
kuwa wanaohusika na utaratibu huo ni wale waliyotambuliwa na kuorodheshwa
katika maeneo maalumu.
Alisema, juzi Mngurumi aliyataja maeneo husika kuwa ni Kariakoo, Karume, Bunguruni, Mombasa, Jangwani,
Kibasila, Banana na Gongolamboto.
Wafanyabiashara hao wanatakiwa kwenda kwenye maeneo
yaliyotengwa kwa ajili yao ambayo ni Kigogo Fresh, Kivule, Soko la Tabata
Muslim na eneo lililoko mkabala na gereza la Ukonga.
“Huu utaratibu wa kuwatambua wenzetu ulifanyika lini kwani
hatujui siku wala mwaka uliyofanyika wakati ili paswa nasi pia tuorodheshwe
kama ilivyokuwa kwa wafanyabiashara wenzetu,”alisema Rajab.
Daniel Khamis, alisema serikali inapaswa kujenga mazingira
bora ambayo yatawawezesha vijana kufanyabiashara zao bila ya kuingia kwenye mivutano
ambayo inaweza kuwafanya wananchi waichukie serikali yao.
“Tunaomba sehemu na sisi tutengewe eneo kwa vile
watakapoanza operesheni ya kuwaomdoa wafanyabiashara katika hayo maeneo ambayo
siyo rasmi hata sisi tunahusika lakini ndiyo hatujui tunakwenda wapi,”alisema
Khamisi.
Juzi wakati akizungumza na vyombo vya habari, Mngurumi,
aliwataka wafanyabiashara hao kuondoka kwa hiyari yao katika maeneo ambayo siyo
rasimi hadi jana.
Alisema kwa wale watakaokaidi agizo hilo, hataua kali
zitachukuliwa ikiwemo kuchukuliwa bidhaa zao na kupelekwa mahakamani na kupigwa
faini.
No comments:
Post a Comment